Ndege ndogo ya shirika la ndege la tara Airlines iliyokuwa na watu 23
wakiwemo watoto imepota ikiwa maeneo ya usawa wa milima Magharibi mwa
Nepal.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, Magharibi mwa Mji Mkuu
Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima
ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.
Ripoti zinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana ingawa hakuna taarifa zozote kuhusu vifo au majeruhi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na maafisa
wa udhibiti wa safari za ndege wa Pokhara dakika 18 baada ya kupaa na
kwamba hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili.
Maafisa wanasema ndege hiyo ya shirika la Tara Airlines ilikuwa na
marubani watatu na abiria 20, mmoja wao raia wa China na mwingine wa
Kuwait. Wawili kati ya abiria waliokuwa wamebebwa na ndege hiyo walikuwa
watoto.
Tangu mwaka 1949, kumetokea zaidi ya ajali 70 zilizohusisha ndege za kawaida na helikopta, na vifo vya watu 700
0 comments:
Post a Comment