Mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C.
Stori: Mayasa Mariwata, WikiendaDar es Salaam: Inauma sana! Baada ya kuwepo kwa madai kuwa mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C’ amerudia matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kiliingia mzigoni kujua kama anaendelea na dozi ya kuacha ishu hiyo na kujua anakopatia ulevi huo kwa sasa.
Katika kusaka majibu ya mambo hayo mawili, yalipatikana madai kuwa kwa sasa ameacha kwenda kuchukua dozi ya kupona ya Methadone kwenye Hospitali ya Mwanayamala, Dar kama alivyokuwa akifanya awali.
Habari zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vyetu zilieleza kwamba, msanii huyo ambaye tangu alipoanza kupatiwa matibabu ya kuacha unga alikuwa akihudhuria hospitalini hapo kuchukua lakini sasa haendi.
Ili kung’amua ukweli wa madai hayo, OFM ilizama kwenye Hospitali ya Mwananyamala na kuongea na Mganga Mkuu, Dk. Delila Moshi aliyethibitisha Ray C kutofika tena hospitali hapo kwa ajili ya kupatiwa dozi.
“Ray C haji tena hapa siku hizi labda amehamia Muhimbili,” alisema Dk. Delila.
OFM ilifika Muhimbili ili kujua maendeleo ya mwanadada huyo ambapo Afisa Habari aliyejitambulisha kwa jina moja la John alidai kuwa Ray C si miongoni mwa watu waliohamishiwa hapo.
“Kuna wagonjwa wamehamishiwa hapa lakini Ray C hayupo,” alijibu kwa kifupi na hata alipobananishwa kuwa mwanadada huyo amehamishiwa hapo na huenda ameamua kuacha dozi aliishia kucheka.
Katika fukunyuafukunyua, OFM ilipokea madai kwamba, baada ya kuacha dozi kwa sasa ana machimbo yake ambayo huwa anakwenda kununua unga.
Katika hilo, yalitajwa maeneo mawili, Magomeni na Mwananyamala nyuma ya hospitali hiyo.
OFM ilifika maeneo hayo yote na kushuhudia pilika za watu wasioeleweka huku wakijishtukia na kumshangaa Kamanda wa OFM, wakiambizana kuwa kulikuwa na sura ngeni katika maeneo yao hivyo wachukue tahadhari.
Kwenye eneo hilo la Mwananyamala, OFM ilibaini nyumba moja iliyodaiwa kuwa ndilo chimbo la ‘mambo hayo meupe’.
Katika kujiridhisha na mzani wa habari hiyo, OFM ilimtafuta Ray C ili kueleza juu ya madai ya kuacha tiba hiyo huku akitajiwa maeneo anayokwenda kuchukua unga ambapo aliwaka akidai kwamba hajaacha kwenda kuchukua dozi Mwananyamala.
0 comments:
Post a Comment