(Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. )
***
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick
Shoo ameitahadharisha Serikali kuhusu zoezi la Utumbuaji Majipu
linaloendelea akiitaka kuzingatia misingi ya haki na busara ya Ki-mungu
ili kutowapa nafasi watu wasio waaminifu kuitumia vibaya kufanya
ukandamizaji.
Askofu
Shoo aliyasema hayo jana mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, katika ibada
maalum ya kuingizwa kazini iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
Alisema
kuwa Kanisa lina imani na Serikali ya Awamu ya Tano na kupongeza juhudi
zake katika kupambana na watumishi wa wanaojihusisha na ubadhirifu wa
mali za umma pamoja na mafisadi, lakini zoezi la kutumbua majipu
linapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka uonevu.
“Utumbuaji
huu ufanyike katika misingi ya haki na kwa busara kwani watu wengine
wanaweza kutumia mwanya huu kuonea wenzao wasiokuwa na hatia,” alisema Askofu Shoo.
Katika
hatua nyingine, Askofu Shayo alielezwa kusikitishwa na vitendo vya
utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya wabunge wanapokuwa Bungeni.
“Tunahitaji
kuona Bunge linajadili vikao vyake kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi
ya demokrasia. Kanisa linasikitishwa sana na vitendo vya utovu wa
nidhamu vinavyoendelea bungeni. Tunapenda kuona hoja zinajadiliwa kwa
ustaarabu,” alieleza.
Kadhalika,
Askofu Shayo aliionya matumizi ya jeshi la Polisi ndani ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza kuwa Bunge ni sehemu ya
Demokrasia na kamwe haipaswi kulindwa na jeshi. Aliongeza kuwa Bunge
linapaswa kuendeshwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na uwazi.
Aliihakikishia
serikali kuwa Kanisa litaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ikiwa
ni pamoja ikiwemo sekta ya elimu na afya. Aliishauri Serikali kuangalia
upya sera ya elimu bure na kuboresha utoaji wa elimu hiyo.
Naye
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizishukuru taasisi za dini kwa
kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kupitia sekta
mbalimbali na kuzihimiza kuendelea kuwekeza katika maeneo muhimu
yakiwemo ya Afya na elimu.
“Napenda
kutumia fursa hii kuyashukuru madhehebu ya dini ambayo yamekuwa mstari
wa mbele kusaidia Serikali katika kufikisha huduma hizi za afya karibu
zaidi na wananch. Wito wangu kwa hili, naombeni mjitahidi kutoa huduma
hizi kwa gharama nafuu ili wananchi wengi waweze kuzitumia,” Waziri Mkuu Majaliwa ananukuliwa.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
0 comments:
Post a Comment