SHUHUDA
Ishu
ilikuwa hivi, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda
Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki
road.
Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana. Nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.
Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puuu! puuu! pooo! poooo! poooo! kama risasi 6 au 8 hivi – kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote.
Majambazi
wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni
wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja.
Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwaspeed ya 220.
Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu. Yaani ilikuwa kama Movie
0 comments:
Post a Comment