Sunday, 20 January 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 57

...
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Nikasimamisha gari kwenye mitimiti kadhaa, tukashuka kwenye gari na Ethan akanisogogelea na kunishika mkono wangu wa kulia na kuniambia kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuniona nikitembea katika eneo hili. Tukapandisha hadi gorofa ya tano, nikaanza kusikia vilio vya mtu akigugumia kulia kwa kipigo anacho kipokea kutoka kwa mtu anaye mpiga. Tukaingia kwenye chumba hicho, sikuamini macho yangu mara baada ya kumkuta baba mke, Biyanka pamoja na walinzi wapatao kumi huku Biyanka akimpiga kijana huyo kwa rungu kubwa.
“Niliwakanya mucheze na kote ila si kucheza na mume wangu. Kama muna fanya kazi chini ya baba yangu mufanye tu ila si kumgusa mume wangu sawa wewe mwana haramu”
Biyanka alizungumza  huku akihema, akafuta jasho linalo mtiririka usoni mwake, kisha akaandelea kumshushia marungu kijana huyu huku baba yake akitabasamu kwa binti yake kuifanya kazi hiyo ya kikatili sana.
   
ENDELEA
“Huyu ndio mke na baba mkwe anaye tarajia kuwa raisi wa hii nchi”
Ethan alizungumza kwa sauti ya chini kidogo, hapakuwa na mtu aliye weza kusikia sauti yake wala kuona uwepo wetu ndani ya hichi chumba.
“Yule binti hakikisheni kwamba muna muua mume nielewa?”
Nikastuka tena mara baada ya kuisiki sauti hiyo ya Biyanka akiwaamrisha vijana hawa.
 
“Sawa madam”
“Endapo yule binti atakuja kutoa ushahidi juu ya baba yangu, vichwa vyemu mimi mwenyewe ndio nitavikata”
“Tumekuelewa Madam”
Biyanka akalitupa gongo alilo lishika chini na kutoa noti kadhaa za shilingi elfu kumi kumi na kumtupia jamaa aliye kuwa anapiga.
“Nenda hospitali na ufunge domo lako”
“Asante sana madam”
Siri ya kumfahamu Biyanka kuwa nii mtu wa hatari, sasa nimeigundua, siri ambayo imezaa chuki na hasira mpya dhini ya yeye na familia yake.
“Wanamzungumzia binti gani?”
Nilimuuliza Ethan huku nikimtazama usoni mwake.
“Clara”
“Nini….!!?”
 
“Ndio maana yake, ile ni kesi ya bucha ukampelekea fisi.”
“Una maana gani?”
“Afande Kimaro anafahamu mchezo mzima na yeye ndio aliye muagiza binti huyo kwenda kuwaua vijana wake. Hujiulizi ni nani ambaye alikuwa anafahamu kwamba mulimpeleka pale Clara na ndani ya muda mchache wameuwawa?”
Maswali haya mfulilizo ya Ethan yakaanza kujenga picha moja kichwani mwangu ya kuchezewa.
“Umshukuru Mungu kwamba ulipata akili ya kuzima simu yako na laiti usinge izima basi wangekutafute kule ulipo kuwa na unakula bata na watoto wazuri wazuri”
Ethan alizungumza huku akitabasamu. Biyanka, baba yake pamoja na walinzi baadhi wakatupita pembeni yetu pasipo kuweza kutuona. 
 
“Hawa walinzi wa mwisho wawili ndio wataletwa kukulinda , itabidi uwe wakali”
“Nitawakataa?”
“Wala usiwakatae”
“Lazima niwakatae kwa mana kama mke ni bomu unahisi hawa nao watakuwa ni kitu gani kwa maana hapa watakuwa wamenizunguka mimi”
“Usijali katika hilo kumbuka kwmba mimi pekee ndio ninaye kulinda. Hao watakuwa wanafanya kazi bure tu kwako”
“Mmmm na mtoto wa watu je?”
“Clara nitakwenda kumchukua. Nitamtafutia sehememu uweze kumficha bila ya wao kuweza kufahamu, ila siku ya siku mambo yatakapo bunduluka basi atakuwa ni shaidi namba moja kuhakikisha kwamba ana muangusha madarakani adui yako”
 
“Ushahidi atautoaje?”
“Wewe zubiri uone”
Tukatoka ndani humu na kuwakuta Biyanka na walinzi wake wakiingia kwenye moja ya gari na kuondoka huku baba yao akiingia kwenye gari jengine na walinzi wake na kuondoka eneo hili. Tukaelekea lilipo gari langu na kuanza kurudi hotelini. Nikafika hotelini na kuchukua kadi yangu ya kufungulia mlango, moja kwa moja nikapitiliza hadi chumbani kwangu huku kichwa changu nikihisi kikiwa kimevurugwa kisawa sawa.
“Namuacha huyu mwanamke”
“Unakwenda kuharibu kila kitu. Wakati wako wa sasa si wakumuacha”
 
“Unataka nikae na jini kweli?”
“Mimi ni nani?”
“Ohoo samahanishi jini kama jini. Namaanisha mwanamke mwenye roho mbaya”
“Kuna msemo wa kuwa muwinda hugeka kuwa muwindaji”
“Una maanisha nini?”
“Wao hadi sasa hivi hawajui kuwe wewe ni adui yao mkubwa. Wanacho jua ni kukuzuia katika kusaidia Clara wakihisi kwamba ndio njia sahihi ya kumtoa mbele ya uso wako”
“Ohoo Mungu wangu”
 
“Jambo ambalo ninakwenda  kukueleza ni juu kuwa makini na wale mabinti wawili. Qeen na Latifa”
“Kwani ni wasaliti?”
“Hakuna ambaye atakwenda kukusaliti”
“Ila?”
Ethan akazungusha kiganja chake cha mkono wa kulia juu ya tumbo lake.
“Sijaelewa?”
“Angalia usije ukawapa mimba na mbaya zaidi wamekupenda kutoka kwenye mioyo yao na wameridhika kuwa na mwanaume mmoja kimapenzi”
“Heeee!”
“Ndio wewe shangaa ila huo ndio ukweli wa mambo unao endelea kwenye mioyo yao”
“Sawa nimekuelewa, ila tuachane na wao kwa sasa naomba umtafute Clara”
 
“Usijali, kesho mchana muda wa chakula nitakuchukua ukamuone sehemu nitakapo muhifadhi”
“Nitashukuru, ila kuna muunganiko gani kati ya Clara na muheshimiwa Poul Mkumbo?”
“Muunganiko uliupo ni kwamba baba Clara na Poul walikuwa ni marafiki wakubwa sana. Ila Baba Clara alikuwa ni rafiki mwema kwa rafiki yake, ila Mkumbo hakuwa mwema kwa mwenzake. Clara aliweza kumshuhudia mkumbo akimbaka mama yake  na kumpa onyo kwamba endapo atazungumza chochote atamuua”
“Mmmmm”
“Mkumbo hakuishia hapo akapanga mpango mzima wa kumuua rafiki yake pamoja na yule kijana aliye kamatwa, baba mdogo wa Clara, na siku ule mpango unapangwa Clara aliweza kuusikia na aliweza kuurekodi kwenye karedio kake kadogo ka taple, ambacho amekificha sehemu anayo ijua yeye mwenyewe”
 
Maneno ya Ethan yakanikumbusha kipindi wazazi wangu walivyo kuwa wana uwawa na vijana wa mkumbo huku mimi na mama tukiwa tumejificha kwenye migomba.
“Huyu mzee ni mwana haramu sana”
“Ni zaidi ya mwana haramu, mimi nina ondoka tutaonana kesho”
“Sawa”
“Ila usizungumze kitu cha aina yoyote kwa Biyanka”
“Nimekuelewa”
Ethan akatoweka kwenye upeo wa macho yangu na kuniacha peke yangu humu chumbani. Nikavua nguo zangu zote na kupanda kitandani na kulala.
                                                                                                                              ***
    Kengele ya mlangoni ikanistua kutoka usingizini. Nikautazama mlango wa chumba changu kwa sekunde kadhaa kisha nikashuka, nikachungulia kwenye kishimo kidogo na kumuona Biyanka akiwa amevalia vizuri sana. Nikafungua mlango na taratibu akaingia huku akiwa amejawa na tabasamu. Akanikumbatia na kunibusu mdomoni mwangu kama si yeye aliye toka kufanya tukio la ujambazi.
 
“Umeshindaje mpenzi wangu”
“Salama, vipi”
“Safi, mwili wako mbona ni wa moto?”
Biyanka alizungumza huku akiniwekea kiganja chake kimoja kwenye shingo.
“Nahisi ni uchovu wa kulala ila mwili utakaa sawa”
“Mmmm kama una umwa twende hospitalini mpenzi wangu”
“Nipo sawa”
“Sasa hivi ni saa mbili, una onaje leo tukatoka chakula cha usiku mpenzi wangu”
Nikamtazama Biyanka kwa sekunde kadhaa kisha nikamkubalia kwa kutingisha kichwa. Nikaelekea bafuni na kuanza kuoga, nikarudi huku nikiwa nimeshika taulo la kujifutia maji mkononi mwangu. Biyanka akalichukua  taulo hili na kuanza kunifuta, kila nikimtazama usoni mwake nina likumbuka tukio alilo kuwa ana lifanya.
 
“Ulikuwa wapi?”
Nilimuuliza Biyanka huku nikimtazama usoni mwake kwa macho ya kumdadisi.
“Nilikuwa nyumbani kwa mama”
Nikatamani kumshushia tusi kubwa ila nikajikaza moyo wangu.
“Anaendeleaje mama?”
“Aha…salama ana kusalimia. Pia baba anasehema kwamba analishughulikia swala lako la kutishiwa pia niliweza kumueleza juu ya Clara na akasema kwamba yote atayafanyia kazi”
 
‘Jamani mbona umekuwa muongo wewe mwanamke?’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama Biyanka usoni mwake.
“Nitashukuru, nitolee pensi na tisheti ile ya kijivu ndio najisikia kuvaa usiku wa leo”
“Poa mume wangu”
Nikachukua simu yangu na kuanza kuikagua, nikatamani kuwatumia meseji Biyanka na Qeen ila nikajizuia, sihitaji kuwaingiza matatizoni watoto wa watu. Nilipo maliza kuvaa, tukatumia gari la Biyanka kuondoka eneo hili huku walinzi wakitufwata nyuma na gari lao. Tukafika katika moja ya hoteli ambayo sikumbuki hata jina lake lililo andikwa nje.
 
“Ethan unaonekana una mawazo sana mpenzi wangu”
“Kichwa changu kwa leo hakipo vizuri”
“Tambua baba yangu ana shuhulikia kija jambo mpenzi wangu kuwa na amani na kesho anakwenda kuwaleta wale walinzi alio kuahidi”
Nikafumba macho ili kuzuia hasira yangu, kwani hao watu ninao letewa naamini watakuwa ni wachunguzi kwangu, nikashusha pumzi taratibu na kumtazama Biyanka ambaye taratibu akausogeza mikono yake na kunishika mikono yangu.
“Tambua kwamba familia yetu inakupenda sana Ethna ipo tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha kwamba kila kitu kina kwenda vizuri kwenye maisha yako”
“Nashukuru”
“Tena nina wazo mpenzi wangu. Hivi kodi ya pale hotelini si inaisha mwezi ujao?”
“Ndio”
“Unaonaje ukahamia nyumbani kwangu na tukaishi pamoja”
“Nitalifikiria ila mwishoni mwa mwezi ujao nitakwenda Ujerumani kufwatilia baadhi ya kampuni zangu”
 
“Unaonaje tukaenda wote?”
“Nani atasimamia kampuni yangu?”
“Si kuna mameneja wengine mume wangu”
“Wewe utasimamia”
Nilizungumza kwa jazba kidogo na kumfanya Biyanka kukaa kimya na kukubaliana na kile nilicho kizungumza. Baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku tukarudi chumbani. Biyanka akaanza uchokozi wa kunishika shika mwili wangu. Kusema kweli hata ile hisia ndogo niliyo kuwa nayo kwake imenipotea kabisa.
“Aiisii…ohooo tamu baby”
Biyanka alizungumza huku akiichukua mikono yangu na kishikisha kiuno chake
 
“Mume wangu kuwa nami, sijakuzoea kukuona hivi”
“Sawa”
Nikaanza kuvuta hisia za mautundu ambayo nilikuwa nina fanyiwa na Qeen pamoja na Latifa, sikumaliza hata dakika tano nikajikuta nikifika kileleni na mchezo ukaishia hapo, sikujali kama Biyanka amefika kileleni au laa. Taratibu Biyanka akashuka juu yangu huku akiwa mnyonge sana, sikuhitaji kumsemesha kitu chochote zaidi ya kugeukia pembeni na kuulazimisha usingizi.
 
“Ethan nahitaji tuzungumze kidogo”
“Tutaonge kesho”
“Nakuomba mume wangu”
“Hivi nikisemea kesho hunielewi Biyanka? Akili yangu imechoka nakuomba uniache bwana”
 
Nilizungumza kwa ukali sana na Biyanka hakuwa na namna zaidi ya kutii. Masaa yakazidi kukatika pasipo sisi wawili kulala kama tulivyo zoeshana, kwani nilizoea kumkumbatia Biyanka kwa nyuma. Sikupata usingizi kabisa hadi kuna pambazuka. Tukaamka na kujiandaa kwa ajili ya kelekea ofisini.
 
“Kazi njema mume wangu”
Biyanka alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu na kuelekea ofisini kwake. Nikaingia ofisini kwangu, kama kawaida, jumatatu huwa kuna ripoti nyingi ambazo kama mkurugenzi ninatakiwa kuzipitia ili niweze kujua ni kitu gani kinacho endelea. Nikawatumia meseji ya Qeen na Latifa, nikiwaomba muda wa mchane nikakutane nao mwenge ili niweze kuongozana nao kuelekea alipo fichwa Clara. Kila mmoja akanijibu  atakuwa tayari japo sijawaeleza ni wapi tunakwenda. Mlango wa ofisini kwangu ukafunguliwa na Biyanka akaingia, akayatazama mafaili yaliyo jazana ofisini kwangu.
 
“Mume wangu hujafanya kazi leo?”
“Ndio”
“Ohoo unaonaje ukaenda hotelini ukapumzike na mimi niweze kushuhulika na hii kazi hapa kwani ofisini kwangu nimesha maliza kila jambo”
‘Usiende sehemu yoyote huo ni mtego’
Niliisikia sauti ya Ethan ikinikanya kwa ukali sana, jambo lililo nifanya nibaki nimekodelea macho Biyanka na kushindwa kumjibu kwani sifahamu ni mtego gani ambao mwanamke huyu amekusudia kuniwekea.

-==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI http://bit.ly/2szzoL5
via Malunde
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger