Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Singida kabla ya kuanza ziara ya uhamasishaji wa kuogesha ng'ombe katika kijiji cha Mgori.
Bw.Rashid Mandoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega.
Bw.Elia Digha,Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida akitoa ujumbe kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (hayupo pichani)kuhusu kuweka mikakati katika sekta ya mifugo nchini.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akikagua ng'ombe katika kijiji cha Mgori kilichopo Singida vijijini alipokuwa ameenda kuzindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Baadhi ya ng'ombe wakisubiri kuogeshwa dawa katika josho la Mgori katika hamshauri ya wilaya ya Singida vijini ambapo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alizindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akichanganya dawa za kudhibiti magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Mgori kwa ajili ya kuhamasisha kuogesha ng'ombe katika majosho yalipo nchini ambapo Serikali imeamua kutoa dawa bure kwa wafugaji.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akisaidiana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo katika josho lenye dawa ambazo zimetolewa bure na Serikali zoezi hilo la uzinduzi katika mkoa wa Singida lilifanyika katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
........................
Na.Alex Sonna,Singida
Serikali imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kudhibiti magonjwa ya mifugo huku ikiwahimiza wafugaji kuzingatia matumizi ya majosho yenye dawa.
Akizungumza na wafugaji Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega wakati wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji wa ngo’mbe kanda ya kati mkoani Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.
Katika uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji kufanya zoezi la uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu, kwa vile hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho yenye dawa ya kudhibiditi kupe.
Aidha amesema kuwa kwa sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa bure kwa halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi kazi, ili wafungaji waweze kuogesha mifugo yao , kukinga ugonjwa hatari unaoenezwa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa nchini.
"Mwanzo shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa ,kutofuata taratibu nzuri za makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata huduma za kuongesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na hivyo kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi yalisimama kufanya kazi"amesema Ulega
Katika kampeni hii ya uhamamishaji wa uongeshaji wa mifugo tozo imepunguwa ambapo hivi sasa kila ng’ombe ana ogeshwa katika majosho ni shilingi 50 tu, huko nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilingi mia 2 kwa kila ngo’mbe na kwa mbuzi ilikuwa shilingi 10.
“Nyie wafugaji msikalie rasialimali hii ya mifugo mliokuwa mnayo, kwani ni uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili kuongeza mapato, yanayotokana na mifugo yenu”amesisitiza Ulega.
Aidha alifafanua kuwa ufungaji kwa kufuata taratibu za ufugaji wa kisasa na kibiashara kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo, itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia.
Uhamasishaji huu unafuatia uzinduzi wa kampeni ya uogeshaji wa mifugo,iliyofanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina katikati ya mwezi jana katika kijiji cha Buzirayombo halmashauri ya chato.
0 comments:
Post a Comment