Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imemhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.” CAG amehojiwa mapema leo Januari 21, 2019 ambapo mara baada ya mahojiano hayo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amesema atawaeleza waandishi wa habari kilichojiri katika kikao hicho. Prof. Assad ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati akijibu swali la mwandishi wa televisheni ya UN, Anord Kayanda kuhusu kutoshughulikiwa ipasavyo kwa ripoti zake zinazoonyesha ufisadi. “Kama tunatoa ripoti na…
0 comments:
Post a Comment