Msanii wa muziki nchini Marekani, Chriss Brown na wenzake wawili wamekamatwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa ya ubakaji.
Tukio hilo limetokea mchana huu Jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwa kwenye uchunguzi wa tuhuma za kudaiwa kumbaka binti wa miaka 24 ambaye alikutana naye katika maeneo ya starehe ya usiku, Januari 15.
Mwanamke huyo alimfungulia mashtaka Chriss Brown akilalamika kumfanyia kitendo hicho cha kikatili, alipomualika chumbani kwake akiwa na mwanamke mwenzake, lakini alipokuwa akitoa maelezo yake alienda mwenyewe chumbani na kukutwa na tukio hilo.
Pia mwanamke huyo aliieleza polisi ya Ufaransa kuwa hata walinzi wa msanii huyo mwenye kipaji cha aina yake walimnyanyasa, na ndipo polisi ikaanzisha uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Mpaka sasa Chriss Brown hajatoa kauli yoyote juu ya tuhuma hizo, na bado yuko nchini Ufaransa ambako alikuwa na ziara.
0 comments:
Post a Comment