Thursday, 9 May 2019

Iran yatishia kurejea katika matumizi ya nyuklia

...
Baraza la Usalama la Taifa la Iran limeamua kusitisha mara moja baadhi ya ahadi zake ilizozitoa chini ya mkataba wake wa nyuklia na nyengine katika siku 60 zijazo, iwapo hakutakuwa na hatua zozote kushughulikia mkwamo wa kiuchumi unaolikabili taifa hilo. 

Katika barua yake kwa mataifa yaliyoendelea kusalia kwenye makubaliano hayo ambayo Marekani ilijitoa, Iran imelalamikia kusitasita kwa makampuni ya mataifa hayo kufanya biashara nayo. 

Viongozi wa China, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Urusi wamepokea barua hiyo, lakini walengwa zaidi ni viongozi wa mataifa ya Ulaya walioshindwa kutimiza ahadi zao ambazo zingesaidia kufufua uchumi wa Iran. 

Wataalamu wameliambia shirika la habari la AFP kwamba mkataba huo wa nyuklia unazitaka nchi zilizoweka saini kuimarisha uchumi wa Iran, lakini makampuni ya nchi za Ulaya bado yanaogopa kufanya biashara na Iran kwa hofu ya kuwekewa vikwazo na Marekani.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger