Thursday, 30 May 2019

Picha : DC MBONEKO AFUNGA MASHINDANO YA UMISSETA MKOANI SHINYANGA... ASISITIZA VIJANA KUBEBA MAKOMBE KITAIFA

...



Na Marco Maduhu - Malunde1 blog 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amefunga rasmi mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA 2019) Mkoani Shinyanga, na kuwataka washindi watakaoungana na kuwa timu moja ya mkoa, wakashiri kikamilifu katika mashindano hayo ngazi ya kitaifa huko Mtwara, na kupata ushindi wa makombe mengi.


Mashindano hayo ya (UMISSETA) yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack Mei 27, 2019 ambapo yamefungwa leo Mei 30 na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwenye viwanja vya CCM Kambarage mjini humo, ambapo washindi wamepewa zawadi  za makombe.

Mashindano yalishirikisha timu mbalimbali kutoka halmashauri ya Kahama Mji, Msalala, Ushetu, Kishapu, Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga  kwa kuchezwa mpira wa miguu, kikapu, pete,tenesi, wavu, riadha, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya.

Akizungumza wakati akifunga mashindano hayo,Mboneko  amewataka washiriki ambao watachaguliwa kuwa timu moja za kwenda kushiriki (UMISSETA) ngazi ya kitaifa, wawe kitu kimoja na kutobaguana kuwa huyo anatoka halmashauri nyingine, bali washindane kama timu moja ambayo inatoka mkoani Shinyanga na hatimaye kuibuka na ushindi.

“Nawapongeza wanafunzi wote mlioshiriki kwenye mashindano haya ya (UMISSETA) ambapo mmeonyesha vipaji vyenu na wote ni washindi, lakini hamtaweza wote wanafunzi 704 kwenda kushiriki ngazi ya kitaifa, bali tutachagua wanafunzi 120 ili wakatuwakilishe na tunataka mrudi na makombe mengi,” amesema Mboneko.

“Na mtakapokuwa kambini muwe timu moja na kutobaguana kuwa huyu anatoka halmashauri hii, sitaki kitu kama hicho bali nataka muwe ndugu kwani nyie wote mnatoka Shinyanga, na mkashindane kweli kweli kwa kuonyesha vipaji vyenu na kuupatia sifa mkoa wetu,”ameongeza.

Pia amewataka washindi ambao watachaguliwa kwenda kushiriki mashindano hayo ngazi ya kitaifa, wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu na siyo kwenda kuchafua sifa ya mkoa.

Naye Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi, amewataka wanafunzi hao pindi watakapokuwa huko Mtwara, waonyeshe vipaji vyao ikiwa michezo ni ajira kwa sasa.

Aidha washindi waliopatikana kwenye mashindano hayo ya (UMISSETA) Mwaka 2019 mkoani Shinyanga, mpira wa miguu wavulana ni halmashauri ya Msalala, wasichana halmashauri ya Shinyanga, mpira wa mikono (Handball) wavulana  Manispaa ya Shinyanga, wasichana Kishapu, Volleyball  Manispaa ya Shinyanga, wasichana halmashauri ya Shinyanga.

Kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana na wasichana washindi ni kutoka halmashuri hya Shinyanga, mpira wa pete Kahama Mji, Tenesi mshindi wavulana na wasichana ni Halmashauri ya Shinyanga , riadha wavulana Shinyanga, wasichana Kishapu, ngoma kutoka Ushetu, kwaya Kahama Mji, usafi na nidhamu wavulana Kahama Mji, wasichana Shinyanga.

Hata hivyo katika mashindano hayo ya UMISSETA (2019) Mshindi wa jumla alitoka halmashauri ya Shinyanga , huku kauli mbiu ya mwaka huu inasema ‘MICHEZO NA SANAA KWA ELIMU BORA NA AJIRA.’

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifunga rasmi mashindano ya michezo ya UMISSETA 2019 na kuwataka washindi ambao wamechaguliwa kushiriki ngazi ya kitaifa wakawe kitu kimoja na kupata ushindi wa makombe mengi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akiwataka wanafunzi ambao wamechaguliwa kwenda Mtwara kwenye mashindano hayo ya (UMISSETA) wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifungua fainali ya mashindano ya (UMISSETA 2019) kati ya timu ya mpira wa miguu Kahama Mji na Msalala huku kwa upande wa wasichana ni Kahama Mji na Shinyanga , na kuwataka wacheze kwa nidhamu kwa kuonyesha vipaji vyao.

Fainali ikiendelea kuchezwa kati ya timu ya Kahama Mji wenye jezi ya njano pamoja na Msalala wenye jezi nyekundu, ambapo hadi dakika 90 zinakamilika walitoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na hatimaye kwenda kwenye matuta ili mshindi aweze kupatikana.

Penati/Matuta yakipigwa ambapo Msalala waliibuka na ushindi wa magoli 4 kwa matatu dhidi ya Kahama Mji na hatimaye kuwa mabingwa rasmi kwa mpira wa miguu katika UMISSETA Mwaka (2019) Mkoani Shinyanga.

Mchezo wa Fainali wa mpira wa miguu ukichezwa kati timu ya wasichana ya Shinyanga wenye Jezi ya Lightblue, na Kahama Mjini wenye Orange, ambapo Shinyanga waliibuka na ushindi wa goli moja na kuwa mabingwa.

Wanafunzi kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiangalia fainali ya michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya (UMISSETA) 2019 Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiangalia fainali ya michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya (UMISSETA) 2019 Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga na kusubiri washindi kupewa makombe yao.

Wadau wakishuhudia fainali ya mashindano ya UMISSETA.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA).

Hamasa zikitolewa uwanjani.

Wanafunzi kutoka Ushetu wakitoa burudani ya ngoma.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisalimiana na wachezaji wa timu ya Msalala kabla ya kuanza kucheza fainali na timu ya Kahama Mji, kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga mwaka 2019 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kahama Mji, kabla ya kuanza kucheza fainali na timu ya Msalala kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga mwaka 2019 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi Kombe kwa mshindi wa mpira wa miguu kutoka halmashauri ya Msalala.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi kombe kwa washindi wa mpira wa miguu kwa upande wa wasichana kutoka halmashauri ya Shinyanga.

Ukabidhiwaji wa makombe kwa washindi ukiendelea kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA mkoani Shinyanga mwaka 2019.

Ukabidhiwaji wa makombe kwa washindi ukiendelea kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga mwaka 2019.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi Kombe kwa mshindi wa jumla kwenye hitimisho la mashindano hayo ya michezo ya UMISSETA Kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Awali makombe yakiandaliwa tayari kwa kukabidhiwa washindi wa mashindano ya michezo ya UMISSETA mkoani Shinyanga mwaka 2019.

Waamuzi nao wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufunga Rasmi mashindano ya michezo ya UMISSETA Mkoani Shinyanga Mwaka 2019.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger