Na Amiri kilagalila-Njombe
Imani za kishirikina mkoani njombe zimetajwa kuwa ndio chanzo cha walimu kukaa kwa muda mfupi katika vituo vya kazi pamoja na wanafunzi kutokufika mashuleni (utoro).
Aidha imeelezwa kuwa kutokana na uwepo wa imani za kishirikina kwa baadhi ya shule zilipo pembezoni mwa mji inapelekea wanafunzi kufanya vibaya katika masomo yao hali ambayo ina athiri kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.
Hayo yamebanishwa na afisa elimu kata ya mlowa Nitson Damian Mkate halmashauri ya mji wa makambako mkoani njombe wakati akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuisha kwa mkutano wa hadhara katika mtaa wa Idofi , amesema kuwa katika kata hiyo kuna mtoto ambaye ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kila anapotaka kwenda shuleni anapatwa na tatizo la kuvimba usoni.
“Ni kweli ushirikina upo lakini ni tofauti na miaka ya nyuma kwa mfano mwaka jana mwalimu mkuu wa shule ya msingi Idofi alichukua walimu wa kujitolea kutoka Lungemba akawaleta hapa lakini usiku walikutana na sintofahamu ambayo hawakujua ni nini,walilala na suruali wakaamka asubuhi suruali zipo nje wengine walilalia mito wakamka asubuhi wakaona mito ina damu lakini hakuna mchubuko wa aina yoyote”alisema afisa elimu
Rajab Shomari ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi idofi amesema licha ya tabia hizo za kishirikina kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwa nitofauti na miaka ya nyuma bado kuna tatizo hilo kwa baadhi ya watoto wanao jihusisha na vitendo hivyo pamoja na wazazi.
“Kuna watoto ambao wana tabia hizo na kuna wazazi ambao pia wanatabia hivyo,kwa miaka ya nyuma kulikuwa na asilimia kubwa sana lakini kwa sasa kutokana na kukemea kemea vitendo hivi vimepungua,kwa upande wa wanafunzi mtoto anaweza akaanguka chini anapoulizwa katika hali ile anataja baadhi ya watu wanaofanya vitendo hivyo sasa inakuwa ngumu kuthibitisha lakini huwa inakuwa hivyo”alisema Shomari
Festo Mwalongo ni diwani wa kata hiyo ya mlowa amesema kuwa imani za kishirikina hazipo katani kwake pekee bali zipo kila mahali ambazo zinasababishwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya jamii na kuwataka walimu waendelee kumtumikia Mungu.
“Habari ya ushirikina sio inaanzia kwenye kata ya Mlowa,sasa hawa watu wachache wanao jihusisha ni kwa kukosa elimu,sasa hivi watu wengi wana nguvu ya Mungu itafika mahala hawa washirikina wataenda nyumba nyingine watateketea kwa moto,sasa sihitaji wakafika mahala wakaanza kutaabika, pamoja na ushirikina huo wawaone wachungaji ili wateketeze huo ushirikina wao”alisema Diwani
Wananchi wa mtaa huo wameitaka serikali kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wananchi hao juu ya uwepo wa imani hizo za kishirikina kwa kuwa zimepelekea kudidimiza shughuli za kimaendeleo katika mtaa huo.
0 comments:
Post a Comment