Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amewataka watanzania Kuwa na desturi ya kusoma kwanza maelekezo yaliyopo kwenye tiketi ya kusafiria pindi wanapotaka kusafiri ili kuondoa migongano na migogoro baina yao na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri.

Mhe.Nditiye ameyasema hayo Mei 30,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa ShauriMoyo Mhe.Mattar Ali Salum aliyehoji juu ya baadhi ya kampuni za usafiri hususan Usafiri wa Majini kwa njia ya Boti kuuza tiketi kwa abiria kwa ajili ya Safari lakini abiria anapochelewa safari tiketi hiyo huwa haitumiki na hivyo kusababisha hasara na usumbufu kwa abiria .
Katika Majibu yake Mhe.Nditiye amesema tiketi ni moja ya mkataba kati ya abiria na mmiliki wa chombo cha usafiri hivyo abiria anatakiwa kusoma kwanza maelekezo yaliyo kwenye tiketi na kama hatoridhika na maelekezo hayo ana ruksa ya kusitisha kukata tiketi ili kuondoa usumbufu.
Hata hivyo,Mhe.Nditiye amesema ufuatiliaji wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kupitia TASAC Umebaini kuhusu changamoto hizo na serikali inalifanyia uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment