Tuesday 28 May 2019

Iran Yasema haioni uwezekano wa mazungumzo na Marekani

...
Iran imesema kuwa haioni uwezekano wa kufanya mazungumzo na Marekani. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za kigeni wa Iran Abbas Mousavi amesema hayo leo, siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kuna uwezekano wa makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa silaha za nyuklia. 

Mousavi amenukuliwa na shirika la habari la Fars akisema kuwa Iran haitilii maanani maneno bali kile ambacho ni muhimu kwa Iran na mabadiliko ya namna suala hilo linavyoshughulikiwa. 

Hapo jana, Rais Trump alisema anaamini kuwa Iran itapenda kuwa na makubaliano na anafikiri hilo ni wazo zuri na kuna uwezekano wa hilo kufanyika. 

Mzozo umezidi kuongezeka kati ya Marekani na Iran tangu Marekani ilipozipeleka ndege zake za kivita na silaha nyingine za vita Mashariki ya Kati, na Rais Trump kutangaza mipango ya kuwapeleka wanajeshi 1,500 zaidi katika eneo hilo, hali ambayo imeibua hofu ya vita. 

Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, na ikaongeza vikwazo dhidi ya Iran.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger