Sunday, 26 May 2019

MAFURIKO YALETA KIZAAZAA BUKOBA

...

Mvua iliyonyesha leo asubuhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera ukiwemo Mji wa Bukoba, imesababisha maafa makubwa ikiwamo kuingia katika makazi ya watu, na madaraja kujaa maji hali iliyosababisha wananchi kushindwa kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine.

Maeneo yaliyozingirwa na maji ni pamoja na Omukigusha, Kyakailabwa, Hamugembe, Buyekera na Kagondo, lakini hadi sasa hasara iliyosababishwa na mvua hiyo bado haijafahamika, huku mali zinazoonekana kuathirika zaidi zikiwa ni nyumba na vitu vya ndani.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba wamesema mafuriko hayo yametokana na baadhi ya wananchi kujenga kandokando ya mito hivyo kubana mkondo wa maji matokeo yake maji kushindwa kutiririka vizuri.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amesema hivi sasa wamezuia wananchi wasijaribu kuvuka kwenye madaraja yaliyojaa maji kwenda popote ili kuepuka madhara zaidi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger