Tuesday 28 May 2019

BOMU LAGUNDULIWA KWENYE GARI KUUZWA KAMA VYUMA CHAKAVU SERENGETI

...

Picha hii haihusiani na tukio.

Bomu lililokuwa linasafirishwa kutoka Serengeti kwenda Mkoa wa Mwanza kuuzwa kama vyuma chakavu limegundulika katika gari la mfanyabiashara wa vyuma chakavu.

Mfanyabiashara huyo mkazi wa Mugumu Serengeti mkoani Mara, Jonas Marwa anasema wakati anapakia mzigo kwenye gari ndipo alipogundua kuwa kuna chuma ambacho sicho cha kawaida kwenye mzigo huo.

Naye Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti, Methiew Mgema anasema, "mara baada ya kuona chuma kisicho cha kawaida, mfanyabiashara huyo alikuja kutoa taarifa kituoni na tukaenda kukagua tukabaini kuwa ni bomu".

Mara baada ya kuliteketeza bomu ilo na maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikosi cha 27, Afisa wa Kikosi hicho, Meja Patrick Kitosi ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu na wananchi wote kutoa taarifa pindi wanapoona vyuma ambavyo siyo vya kawaida.

Bomu hilo linalokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 10, limeteketezwa hadi mwisho mbele ya maafisa hao wa polisi na jeshi.
Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger