Mhubiri mwenye utata James Ng'ang'a wa Kanisa la Neno Evangelism Center nchini Kenya ametishia kuchukua hatua mikononi mwake na kuyafunga matawi mengine ya kanisa lake kwa kile alichokitaja kama kukosewa heshima.
Wakati wa ibada, Ng'ang'a amewaonya waumini, maaskofu dhidi ya kummezea mate mkewe.
Ng'ang'a aliyekuwa mwingi wa hasira aliyataja majina ya baadhi ya waumini wa kanisa hilo la Neno Evangelism Center.
"Mengi yamekuwa yakisemwa. Iwapo mtashindwa kumheshimu mke wangu nitawafukuza katika kanisa hili. Wakati huu sasa nitawaonesha uwezo wangu,You will know my true colour" Ng'ang'a alitishia.
Haijabainika wazi kile mtumishi huyo alimaanisha kwa kutamka kukosewa heshima lakini aliwakemea baadhi ya waumini kwa madai ya kumvizia mkewe.
Hakukomea hapo tu bali alizidi kuwaonya baadhi yao kwamba iwapo hawatabadili mienendo atawachukulia hatua.
"Vile vile, mwanamke yeyote ambaye atamkosea heshima mke wangu nitamfurusha humu kanisani. Utaondoka katika kanisa langu na kuanzisha lako,"aliongeza.
Matamshi yake yaliwashtua waumini kanisani humo, ambao hawakuwa na la kufanya ila kuketi kitako na kumsikiza kwa makini huku wakisalia kumkodolea tu macho.
Machi, 2019 alijipata pabaya baada ya kushtakiwa kwa kumtishia mwanahabari Linus Kaikai wa Citizen TV, baada ya Linus kupendekeza wachungaji wote ni sharti wawe na shahada ndipo wahudumu kama mapasta.
Mhubiri huyo ambaye amezongwa na utata si haba alifunga ndoa na mkewe Mercy Murugi kwenye sherehe ya kifahari ilyoandaliwa Windsor Golf Club na kuhudhuriwa na wanasiasa mashuhuri.
MSIKILIZE HAPA
MSIKILIZE HAPA
0 comments:
Post a Comment