Mgombea Mbunge wa Jimbo la Busega, Simon Songe akichukuwa fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo hilo
Na Woinde Shizza , Busega
Mbunge wa Jimbo la Busega, Simon Songe ameibua matumaini mapya kwa wananchi wa jimbo hilo baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea tena nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, mbunge huyo aliwashukuru viongozi wa chama hicho kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kupitia tiketi ya CCM Aidha, alimshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Kamati Kuu ya chama hicho kwa mwongozo na maono yao ya kuliletea taifa maendeleo.
“Naishukuru sana Kamati Kuu ya CCM ikiongozwa na Mwenyekiti wetu, Mama Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi imara unaoendelea kuimarisha chama na kuwaletea Watanzania matumaini Nimechukua fomu hii nikiwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Busengo kwa uaminifu na mshikamanio wa kweli,” alisema.
Mbunge huyo aliahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi wa Busengo katika kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili zinatatuliwa, ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za umeme vijijini, pamoja na kuboresha sekta ya elimu.
Aliongeza kuwa maendeleo ya Jimbo la Busega ni jukumu la pamoja, hivyo ataendelea kusimama mstari wa mbele kushirikiana na wananchi, serikali na wadau wengine ili kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na matunda ya chama hicho.
Wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo walionyesha furaha na kuahidi kumpa ushirikiano wa dhati katika safari yake ya kuendeleza maendeleo ya jimbo hilo kupitia CCM.
%20(1).jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 comments:
Post a Comment