Saturday, 23 August 2025

CCM YAVUNJA REKODI:SURA MPYA, SURA ZILIZOREJEA NA WALIOSHUKA

...


Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Katika kile kinachotajwa kuwa ni mojawapo ya maamuzi muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi majina ya wanachama wake walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia majimbo mbalimbali na viti maalum.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Agosti 23, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, kufuatia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika kwa lengo la kupitisha uteuzi wa mwisho.

katika mkoa wa Arusha, jina lililovuta hisia za wengi ni Paul Makonda, aliyeteuliwa kugombea Ubunge wa Arusha Mjini – hatua inayotafsiriwa na wachambuzi kama "comeback" ya kisiasa kwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Joshua Nassari, ambaye zamani alikuwa mbunge kupitia upinzani na baadaye kujiunga na CCM, naye amepitishwa kuwania tena Ubunge wa Arumeru Mashariki, hatua inayoonesha msimamo wa chama kuvuta na kuwekeza kwa wanasiasa waliobobea hata kutoka nje ya mfumo wake wa awali.

Majina mengine yaliyopitishwa Arusha ni pamoja na Dkt. Johannes Lukumay – Arumeru Magharibi,Daniel Tlemah – Karatu,Dkt. Steven Kiruswa – Longido,Isack Copriao – Monduli na Yannick Ndoinyo – Ngorongoro.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kuwa eneo lenye mvuto mkubwa kisiasa, na safu ya walioteuliwa mwaka huu inadhihirisha mchanganyiko wa sura zile zile zenye uzoefu wa muda mrefu serikalini na ndani ya chama.

Prof. Kitila Mkumbo, aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Mbunge wa Ubungo, amerudi tena kuwania jimbo hilo.

Aidha, wabunge wakongwe kama Bonnah Kamoli (Segerea), Mussa Zungu (Ilala), na Jerry Silaa (Ukonga) wameendelea kuaminiwa na CCM na kupitishwa tena.

Kwa upande wa vijana, Geofrey Timoth (Kawe) na Kakulu Buchard (Mbagala) ni miongoni mwa sura mpya zilizopitishwa – ishara kuwa CCM inaendelea kujenga kizazi kipya cha wanasiasa.

Majina mengine yote ya Dar es Salaam ni Haran Sanga – Kigamboni,Angellah Kairuki – Kibamba,Prof. Kitila Mkumbo – Ubungo,Mariam Kisangi – Temeke
,Abdallah Chaurembo – Chamazi,Kakulu Buchard – Mbagala,Geofrey Timoth – Kawe,Abbas Gulam “Tarimba” – Kinondoni,Mussa Zungu – Ilala,
Jerry Silaa – Ukonga, Bonnah Kamoli – Segerea na Dougras Masaburi – Kivule

WAONGOZAJI WA KURA ZA MAONI WAKATWA – WAPYA WAIBUKA

Katika hali ya kushangaza baadhi ya waliokuwa vinara wa kura za maoni hawakurejeshwa kwenye uteuzi wa mwisho, hali iliyoacha maswali na mijadala miongoni mwa wanachama.

Waliokosa uteuzi licha ya kuongoza kura za maoni ni pamoja na Ummy Mwalimu – aliyekuwa Mbunge wa Tanga Mjini,Samuel Malecela – mshindi wa kura za maoni Dodoma Mjini

Katika jimbo la Kigoma Mjini, jina lililoibuka ni la Clinton Revocutus maarufu kama Baba Leo, ambaye amepitishwa licha ya kutokuongoza kwenye kura za maoni.

Majimbo mengine yaliyoshuhudia mabadiliko makubwa ni Tarime Mjini – Ester Matiko,Bunda Mjini – Ester Bulaya,Urambo – Magreth Sitta,Vwawa – Exaud Kigahe (Naibu Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara)

WALIOPENYA KWENYE ORODHA YA MABADILIKO

Miongoni mwa waliopenya kwenye uteuzi huo wa mwisho ni
Paul Makonda – Arusha Mjini Nape Nnauye – Mtama,Kangi Lugola – Mwibala,Livingston Lusinde – Mvumi,Isaya Moses – Kongwa (akitwaa nafasi ya Hayati Job Ndugai)


MABADILIKO YA VIONGOZI WA JUU NDANI YA CCM

Katika kikao hicho pia, CCM imetangaza mabadiliko ya kiutendaji ndani ya chama ambapo Dk. Asha-Rose Migiro amepitishwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, akichukua nafasi ya Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye sasa ni mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama hicho.

Kenani Kihongosi ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Amos Makalla. Makalla ametoa wito kwa waandishi wa habari kumpa ushirikiano Kihongosi kama walivyompa yeye.

Joshua Milumbe ameteuliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM

Kutokana na hatua hiyo Wachambuzi wa siasa wanasema uteuzi wa mwaka huu ni wa kuvutia, ukijumuisha mabadiliko ya kizazi, uhamasishaji wa sura mpya na uimarishaji wa uongozi wa chama kwa kuteua viongozi wenye maono mapya.

Pia, uteuzi huu umeashiria juhudi za chama kuongeza uwakilishi wa jinsia na maeneo mbalimbali nchini.










Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger