
"Kazi na Utu, Kishapu Mpya ya Kimataifa"
Bonda William Nkinga ni kiongozi makini, mzalendo wa kweli na mchapa kazi anayeamini katika maendeleo ya vitendo. Akiwa na historia ndefu ya kulitumikia taifa na jamii, Bonda amejipambanua kama kiongozi anayeweza kuibadilisha Kishapu kuwa kitovu cha maendeleo ya kisasa.
🔰 ASILI NA MAISHA YA AWALI
Bonda alizaliwa mwaka 1969 katika Kata ya Ukenyenge, Wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga. Kutoka katika mazingira ya kijijini, alijifunza thamani ya bidii, nidhamu, na mshikamano wa kijamii – misingi inayomfanya leo kuwa kiongozi wa mfano.
🎓 ELIMU NA UMAHIRI KITAALUMA
Bonda ni msomi aliyebobea katika uhasibu na biashara:
👉MBA – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
👉CPA (T)
👉B.COM – Biashara na Uongozi
Mafanikio haya yamemuwezesha kusimamia kwa ufanisi rasilimali za umma na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa uadilifu.
💼 UZOEFU WA KITAALUMA NA KAZI SERIKALINI
Kwa zaidi ya miongo miwili, Bonda amehudumu katika Wizara ya Kilimo kama Mhasibu Mwandamizi akisimamia miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo:
👉Tanzania Agricultural Inputs Support Project (TAISP)
👉Agricultural Sector Development Programme (ASDP)
Amekuwa mstari wa mbele katika usimamizi wa fedha za Serikali na michango ya wahisani wa kimataifa kama Benki ya Dunia, AfDB, na JICA, akihakikisha kila shilingi inaleta matokeo kwa wananchi.
🏛 UONGOZI NDANI YA CCM
Bonda si mgeni kwenye siasa za CCM. Kwa miaka mingi amekuwa nguzo muhimu ya chama katika mkoa wa Shinyanga:
-
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (2012–2022)
-
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Kishapu
-
Naibu Kamanda wa UVCCM – Kishapu (2007–2017)
Kupitia nafasi hizi, amekuwa daraja la kuunganisha chama, serikali na wananchi.
🌍 UONGOZI KATIKA JAMII
Zaidi ya siasa, Bonda ni kiongozi wa kijamii mwenye historia ya kupigania haki na maendeleo ya watu:
👉Mwakilishi wa wafanyakazi – Wizara ya Kilimo
👉Rais wa Serikali ya Wanafunzi SHYCOM (1991–1993)
👉Kilanja Mkuu – Mwadui Sekondari (1989–1990)
👉Mwakilishi wa Wanafunzi – UDSM (1995–1998)
Aidha, alihudumu JKT Kikosi 842 KJ Oparesheni, ambapo alijifunza nidhamu, uzalendo na misingi ya uongozi wa kweli.
🚀 MALENGO YA KISIASA NA KIJAMII
Bonda William Nkinga ana dira ya kulifanya Kishapu kuwa kitovu cha maendeleo:
👉Kuweka msukumo wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo.
👉Kuchochea mapinduzi ya kilimo kwa kutumia uzoefu wake wa kitaalamu.
👉Kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.
👉Kusimamia rasilimali za umma kwa uwazi na uwajibikaji.
👉Kukuza viwanda na sekta za uzalishaji ili kuchangia uchumi wa taifa.
👉Kuwaunganisha wananchi na serikali kwa ushirikiano wa dhati.
🌟 BONDA – KIONGOZI WA VITENDO
Bonda Nkinga anaamini kuwa maendeleo ya kweli yanahitaji kiongozi mwenye maono ya mbali, moyo wa kujitolea, na mshikamano na wananchi. Kwa falsafa yake ya “Kazi na Utu”, anataka kuijenga Kishapu mpya yenye maendeleo ya kimataifa.
📧 Email: bonda.nkinga@kilimo.go.tz
🗳 KISHAPU MPYA YA KIMATAIFA – TWENDE NA BONDA NKINGA!
0 comments:
Post a Comment