Sunday, 22 September 2019

RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI MWINGINE LEO JUMAPILI...KAGUSA PIA TUME YA HAKI ZA BINADAMU

...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  amemteua Jaji mstaafu Methew Mwaimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Jaji Mwaimu anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwanzoni mwa mwaka 2018 baada ya Bahame Nyanduga aliyekuwa mwenyekiti kumaliza kipindi chake cha uongozi.

Rais Magufuli amemteua Mohamed Khamis Hamad ambaye ni Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kuwa Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo.

Rais Magufuli pia ameteua Makamishna wa Tume hiyo kama ifuatavyo; Dk Fatma Rashid Khalfan (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar), Thomas Masanja (Mhadhiri wa Sheria, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino – SAUT) na Amina Talib Ali (Ofisa Mwandamizi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar).

Aidha amemteua Khatib Mwinyi Chande (Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT) na Nyanda Josiah Shughuli (Ofisa Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango).





Balozi Kijazi amesema uteuzi huo umeanza Septemba 19 2019.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger