Sunday, 29 September 2019

Polisi Nigeria Yawaokoa Watu 500 Waliofungwa na Kunyanyaswa Katika Jumba la Mateso

...
Polisi nchini Nigeria imefanikiwa kuwaokoa watoto na vijana kutoka katika kituo kimoja ambacho walikuwa wakifanyiwa mateso.

Maafisa usalama katika jimbo la Kaduna la kaskazini mwa Nigeria wametangaza kuwa, vikosi vya usalama vimefanikiwa kugundua shule moja katika jimbo hilo na kuwaokoa watoto na wanaume 500 waliokuwa wakiteswa kwa mateso mbalimbali kwa ajili ya malengo maalumu.

Vyombo vya usalama vya Kaduna havijaashiria wamiliki wa shule hiyo ingawa vimesema kuwa, wahanga wa mateso hayo walikuwa watoto  na vijana wadogo wa kiume ambao walikuwa wakitumiwa kwa malengo ya kiuchumi.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, vijana hao walikuwa wakiteswa vikali kimwili, kiroho na hata kunajisiiwa.

Wengi wa  wahanga hao ni raia wa Nigeria huku wengine wakiwa ni kutoka katika nchi jirani za Burkina Faso, Mali na Ghana na walipelekwa katika shule hiyo na watu wasiojulikana au wazazi wao kwa ahadi ya kwenda kusoma masomo ya dini.

Tayari polisi ya Kaduna imewatia mbaroni watu wanane kwa tuhuma za kuhusina na mateso dhidi ya vijana hao huku walimu kadhaa wa shule hiyo ambao wanasadikiwa kuhusika katika mateso hao nao wametiwa mbaroni.

Polisi ya Nigeria imetangaza kuwa, imefungua faili la uchunguzi kuhusiana na kashfa hiyo, huku wazazi wa wahanga hao wakipokea kwa mshangao mkubwa habari ya kuteswa watoto wao.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger