Saturday 28 September 2019

TCRA YASHUSHA RUNGU KWA TV ZA MTANDAONI...MILLARD AYO,WATETEZI TV NA KWANZA TV

...

Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu kwa televisheni za mtandaoni kwa kukiuka misingi ya uandishi wa habari na utangazaji na kushindwa kuchapisha sera na mwongozo kwa watumiaji.

Chaneli za mtandaoni zilizokumbwa na rungu hilo ni Watetezi Tv, Millard Ayo na Kwanza Tv ambayo imepewa adhabu ya kufungiwa kwa miezi sita.

Akisoma uamuzi wa kamati Makamu mwenyekiti Joseph Mapunda amesema Kwanza Tv wamekutwa na kosa la kukiuka misingi ya uandishi wa habari na kanuni za utangazaji kwa kuchapisha habari iliyolenga kupotosha.

Amesema kupitia ukurasa wake facebook Kwanza tv iliweka video iliyobebwa na kichwa cha habari Dk Gwajima apata ajali.

Mapunda amesema kwa makusudi habari hiyo haikutaja jina la kwanza la Dk Gwajima hivyo kuzua taharuki hasa ikizingatiwa kuna mtu mwingine maarufu anayetumia jina hilo

Pia Kwanza Tv ilikutwa na kosa la kutochapisha sera na mwongozo kwa watumiaji wake jambo linalowapa uhuru wa kuweka maudhui yoyote bila kujali athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa makosa hayo mawili kamati ilifikia uamuzi wa kuifungia Kwanza Tv kwa muda wa miezi sita.

Kosa la kutochapisha mwongozo kwa watumiaji wamekutwa nalo pia Millard Ayo na Watetezi Tv ambao wote wametozwa faini ya Sh5 milioni na kupewa onyo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger