Sunday, 29 September 2019

Usalama waimarishwa Misri kukabiliana na maandamano dhidi ya Rais Abdul-Fattah al-Sisi

...
Usalama umeimarishwa kote nchini Misri ili kukabiliana na maandamano ya wananchi dhidi ya Rais wa nchi hiyo Abdul-Fattah al-Sisi ambayo yameanza kutishia uongozi wake.

Duru za habari zinaripoti kutoka nchini Misri kwamba, vikosi vya usalama vimepelekwa katika miji muhimu ya nchi hiyo hususan ile ambayo imekuwa mstari wa mbele kwa maandamano dhidi ya Rais Abdul-Fattah al-Sisi.

Wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana kulalamikia matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii wanayokabiliana nayo na kutaka kuondoka madarakani rais wa nchi hiyo Abdul-Fattah al-Sisi baada ya kupita miaka 8 ya vuguvugu la harakati ya wananchi wa Misri lililopelekea kung'olewa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak.

Maandamano hayo yanafanyika kufuatia wito wa Muhammad Ali tajiri Mmisri ambaye yuko uhamishoni nchini Uhispania  baada ya kuweka wazi ufisadi wa kisiasa na kiuchumi wa al Sisi.

Muhammud Ali alituma jumbe kwa njia ya video katikia mitandao ya kijuamii akibainisha kuwa, alikuwa mkandarasi katika jeshi la Misri kwa muda wa miaka 15 na kwamba alimjengea al Sisi jumba la kifahari katika kituo cha kijeshi nchini humo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger