Sunday, 29 September 2019

Hatimaye Mugabe azikwa katika kijiji alikozaliwa

...
Kiongozi mwanzilishi wa taifa la Zimbabwe Robert Mugabe amezikwa Jumamosi katika kijiji alikozaliwa cha Kutama katika eneo la Zvimba na hivyo kuhitimisha mgogoro baina ya serikali na mrithi wake, Rais Emmerson Mnangagwa kuhusu sehemu yake ya kuzikwa.

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliaga dunia Septemba 6 mwezi huu huko nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu.

Awali, serikali ilikuwa imesema Mugabe angezikwa katika makaburi ya mashujaa jijini Harare. Uamuzi huo wa serikali ulikataliwa na familia ya hayati Mugabe. 

Waziri wa Habari nchini humo Nick Mangwana amesema katika taarifa kwamba, serikali imeona ni vema itii matakwa ya familia kuhusu ni wapi mpendwa wao azikwe.

Mugabe ambaye aliiongoza Zimbabwe kwa karibu miongo minne tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka Uingereza mwaka 1980 alilazimishwa kujiuzulu mwezi Novemba mwaka juzi baada ya mapinduzi ya jeshi.

Mugabe alikuwa na mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Zimbabwe na kuiondoa nchi hiyo katika makucha ya mkoloni na hata baada ya uhuru wa Zimbabwe, alisimama kidete kutetea mamlaka ya kujitawala nchi hiyo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger