Sunday 29 September 2019

AUA WAZAZI WAKE KISA WAMEINGILIA MAPENZI ALIYONAYO KWA MREMBO WA TWITTER

...

Mwanaume mmoja raia wa Marekani Grant Amanto (29), mwenye hisia kali za mapenzi dhidi ya mwanamke aliyemuona mtandaoni aliyefahamika kwa jina moja la Sylivia, amewaua wazazi wake pamoja na kaka yake, kwa kile kilichodaiwa kuingilia kati mapenzi yake na mpenzi wake aliyemuona mtandaoni.

Wawili hao hawakuwahi kukutana bali walikuwa wakiwasiliana kupitia mtandao wa Twitter na Skype, ambapo kijana huyo alimlaghai mrembo huyo kwa kujifanya ana uwezo mkubwa wa kifedha huku kiuhalisia alikuwa akiishi katika nyumba ndogo ya wazazi wake, mjini Chuluota, Florida .

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Polisi mjini humo, familia ya Grant ilibaini kijana wao aliiba pesa za mkopo uliochukuliwa na wazazi wake kiasi cha Dola za Kimarekani 150000, na mara baada ya wazazi kugundua hilo walimlazimisha kijana wao amwambie ukweli Sylivia juu ya hali yake ya kipato, ambapo mwenyewe alidai jambo hilo lilikuwa ni udhalilishaji kwake.

Siku ya tukio Grant alianza kwa kumuua Mama yake Marget (61), kisha Baba yake Chad (59) na hatimaye alimaliza kwa kufanya mauaji ya kaka yake Cody (30).

##SOURCE; Mirrow.co.uk news
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger