Saturday, 28 September 2019

Waziri wa Fedha Dk Philip Mpango awasimamisha kazi Maafisa Ununuzi wa Taasisi 6

...
Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango ameagiza kusimamishwa kazi maofisa ununuzi wa Veta, ASA, NIMR, kituo cha Diplomasia na halmashauri ya Wilaya Kaliua na Nsimbo kupisha uchuguzi kufuatia ripoti ya PPRA kuonyesha uzingatiaji hafifu wa sheria ya manunuzi ya umma katika taasisi zao huku akiwataka viongozi wa Taasisi hizo kujipima kama wanatosha katika nafasi zao.

Ametoa maagizo hayo jana akipokea ripoti ya tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka 2018/19 iliyoonesha kuwa kulikuwa na udhaifu wa uzingatiaji wa sheria za manunuzi ya Umma katika Taasisi hizo

Maafisa ununuzi hao ni kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Wakala wa Mbuga za Kilimo, Taasisi ya Utafiti wa Dawa (NIMR), Kituo cha Diplomasia, Halmashauri ya Kaliua na Nsibo

Aidha, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa Taasisi zote ambazo miradi yake haina thamani ya fedha na ile ambayo ripoti inaonesha ilikuwa na viashiria vya rushwa

Miradi ambayo haina thamani halisi ya fedha ni pamoja na mradi wa uchimbaji wa mashimo ya kuchakata taka ngumu wa Halmashauri ya Kahama na usambazaji wa mita za maji katika Halmashauri hiyo hiyo

Baadhi ya Taasisi ambazo miradi yake ilikuwa na viashiria vya rushwa ni Wizara ya Maji, Shirika la Reli Tanzania (TRC), Shirika la viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya majisafi na majitaka, Singida na Wanging’ombe na Manispaa za Kigamboni, Ubungo na Kahama


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger