Sunday 29 September 2019

ROBERT MUGABE AZIKWA NYUMBANI KWAKE

...
Aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amezikwa nyumbani kwake huko Zvimba.

Kiongozi huyo wa zamani aliiongoza nchi yake kujipatia Uhuru lakini baadaye akashutumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu na kuharibu uchumi wa taifa lililokuwa likinawiri.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 95 nchini Singapore mapema mwezi Septemba. Jeneza lake lililokuwa na rangi ya shaba lilishushwa kaburini.

Robert Mugabe alikuwa amezungukwa na mkewe Grace, watoto na watu wa karibu wa familia yake. Ni marafikize wachache wa zamani waliohudhuria mazishi hayo.

Alizikwa katika eneo la nyumba ya familia yake. Ni wachache ambao wangedhania mtu mwenye haiba kama yake angezikwa na watu wachache.

Baadhi wanasema kwamba ilikuwa taarifa yake ya mwisho ya kisiasa. Kitu ambacho kitakumbukwa katika historia ni kwamba Mugabe alikuwa mchezaji wa chess ambaye hakukubali kushindwa

Wakati alipopinduliwa mwezi Novemba aliondoka bila kutaka. Amezikwa mbali na marafikize ambao anaamini walimsaliti.

Baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa.

Katika taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na "matakwa yake [Mugabe]".

Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi atakapozikwa.
Familia yake inasemekana kughabishwa na jinsi kiongozi huyo alivyong'olewa madarakani na mshirika wake, wa zamani Rais Mnangagwa, miaka miwili iliyopita- halia mbayo huenda imesababisha mvutano kuhusu mahali atakapozikwa.

Bw. Mnangagwa alipendekeza kiongozi huyo azikwe Heroes Acre.

Mugabe, alikua Rais wa kwanza wa Zimbabwe baada ya nchi hiyo kupata uhuru 1980.

Miaka ya awali ya uongozi wake, alisifiwa kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu kwa Waafrika walio wengi

Lakini baadae utawala wake ulikumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukandamizaji wa wapinzani wake.

Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2017 na wadhifa wake kuchukuliwa na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.
Je Mugabe ni nani?

Robert Mugabe alikuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe

Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu.

Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali.

Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake.

Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake.

Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000…

Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara katika uchumi.

Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi.

Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza, Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.

Mugabe aliapa kuwa Mungu peke yake ndio angeweza kumtoa madarakani.
Chanzo - BBC
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger