Sunday 29 September 2019

Kabudi: Tanzania tumedhamiria kubadili maisha ya watu wetu

...
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imedhamiria kubadili maisha ya wananchi wake ikijitahidi kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Akihutubia mjadala Mkuu wa Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa kikao cha 74 mjini New York Marekani Ijumaa usiku Profesa Kabudi amesema Tanzania imeweka ajenda kuu za kuzitekeleza ambazo ni pamoja na “kutokomeza ufisadi, kurejesha haki na heshma katika sekta za umma, na kuimarisha ukusanyaji kodi kama mbinu ya kufikiwa kwa haraka ukuaji wa kiuchumi." 

Mengine wanayoyapa kipaumbele ni “elimu bora kwa wote, huduma za afya, na uwajibikaji.”

Waziri huyo amesema  hivi juhudi hizo pia zinalenga kuboresha kiwango cha elimu nchini , kutokomeza umasikini, na kukabiliana na kushughulikia tatizo la ajira, uandikishaji watoto wanaoingia shule kimepanda kwa asilimia 35.2 ikiwa imechangiwa na hatua ya serikali ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi hadi kitato cha nne.

Hatua zinazochukuliwa
Waziri Kabudi amesema serikali imechukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi ambazo ni pamoja na “kuanzisha kitengo cha kupambana na uhalifu na ufisadi katika mahakama kuu, na kuimarisha suala la uwajibikaji na uwazi katika serikali. "

Katika miaka minne iliyopita Profesa Kabudi amesema serikali imetekeleza mabadiliko kadhaa yanayojumuisha kudhibiti utajiri na mali asili ya nchi hiyo kwa kupitia mikataba mbalimbali na hatua hizo zitasaidia kuongeza pato la taifa kwa ukusanyaji mapato, pia sheria mpya za madini zimeisaidia Tanzania kukusanya mabilioni ya fedha ambayo yameisaidia serikali kuongeza kiasi cha bajeti yake hadi asilimia 40 mwaka 2019 ukilinganisha na asilia 25 mwaka 2016.

Profesa Kabudi ameongeza kuwa mapato hayo yamesaidia kuboresha miradi mbalimbali ya miundombinu na kuinua hali ya wananchi kuanzia katika afya, maji, na usafi. Hatua hizo pia zimesaida kutoa elimu bure kwa shule za umma za msingi na sekondari akitolea mfani shule za msingi uandikishaji Watoto umeongezeka kwa asilimia 35.2.

Amesema serikali pia inahakikisha uhifadhi mazingira na kujumuisha kila mwananchi katika mchakato wa SDGs ikiwemo makundi yasiyojiweza.

Na katika upande wa nishati ambayo awali ilikuwa ni bidhaa adimu sasa takriban asilimia 67 ya wananchi wa Tanzania wana nishati ya umeme kutokana na mradi maalum wa kusambaza umeme vijijini, REA .

Pia kuna ujenzi wa bwawa kubwa kabisa la kuzalisha umeme unaoendelea  ambao utakuwa  mkombozi sio tu kwa wananchi wa taifa hilo bali hata nchi jirani.

Pia amesema mbali ya uhifadhi wa mazingira kuna masuala mengine yanayozingatiwa ikiwemo nishati endelevu na kuhakikisha teknolojia hiyo inawasaidia mengi.
Uhuru wa vyombo vya habari

Prosesa Kabudi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uhuru wa vyombo vya habari na kuongeza kiwango cha utoaji leseni akitolea mfano kwamba taifa hilo lina jumla ya vituo vya redio 152 na ni vitatu tu ndivyo vinamilikiwa na serikali, huku vituo vya televisheni vikiwa 34 na viwili tu ndivyo vinavyomilikiwa na serikali. Kwa upande wa magazeti serikali imetoa jumla ya leseni 172.

Na mwisho ametoa wito kwa nchi zote wanachama kukumbatia ushirikiano wa kimataifa sio tu kwa ajili ya kutomoza umasikini, kuboresha kiwango cha elimu, kukabiliana na mabadiliko yatabianchi na kufikia uwajibikaji bali pia katika kudumisha amani na usalama lakini pia katika kuleta haki na kuwa na dunia bora.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger