Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Uvinza, Kigoma, amekutwa na kuku kwenye kizazi baada ya kufika katika kituo cha afya cha Uvinza, akilalamika kuwa anaumwa tumbo na katika uchunguzi daktari akabaini uwepo wa kifaranga hicho ambacho walifanikiwa kukitoa.
Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma, Simon Chacha amesema mwanamke huyo alifika kituoni hapo kupatiwa matibabu akiwa na maumivu makali ya tumbo, “baada ya vipimo na uchunguzi waliona miguu ya kuku katika mfuko wa kizazi wa mwanamke huyo.”
Amesema utaratibu ulifanyika na kufanikisha kutoa kifaranga ndani ya mfuko wa kizazi wa mwanamke huyo.
"Alifika hospitali akadai anaumwa tumbo baada ya uchunguzi madaktari wakaona kifaranga cha Kuku kwenye kizazi na tayari wamekitoa, tukio hilo limefanyika nadhani kwa imani za kishirikina
“Nimeagiza afanyiwe upasuaji ili kujihakikishia zaidi nini kimetokea ”, amesema Dkt. Simon.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kigoma, James Manyama amesema limetokea juzi Desemba 5, 2020 saa tatu usiku katika kituo cha afya Uvinza.
Amesema mwanamke huyo alifika katika kituo hicho akiongozana na mumewe kwa ajili ya kujifungua, walipofika alipitishwa moja kwa moja wodini na mhudumu wa afya wakati akimpatia huduma mwanamke huyo alibaini hali isiyo ya kawaida kutokana na uzoefu wake.
“Alipoona hali si nzuri alimuita daktari wa zamu aliyekuwepo kituoni hapo ili waweze kusaidiana kumzalisha mwanamke huyo. Aliposukuma mtoto kilitoka kiumbe tofauti na mtoto..., alikuwa kuku ambaye hakuwa na manyoya.”
“Tukio hilo ambalo si la kawaida katika jamii zetu linahusishwa na imani za kishirikina ingawa Serikali haina imani na mambo hayo. Polisi litakichukua kiumbe hicho na kukipeleka maabara ya mkemia mkuu mkoani Mwanza kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwani sio kawaida kwa binadamu kuzaa kuku,” amesema Manyama.
==>>Msikilize hapo chini
Video Credit: EATV
0 comments:
Post a Comment