Monday 28 December 2020

RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DED IGUNGA

...
Revocatus Kuuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Revocatus Kuuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli leo Desemba 28, 2020 kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwaa ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.

Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger