Thursday, 19 September 2019

PASTA AWATANDIKA VIBAO WAUMINI MMOJA BAADA YA MWINGINE

...

Pasta James Ng'ang'a wa nchini Kenya ameibuka tena kwa mara nyingine tena na taarifa za kushangaza na pia kufurahisha. 

Mhubiri huyo ambaye taarifa zake huzingiriwa na utata, amewashangaza Wakenya wengi kupitia kwa video iliyosambazwa mitandaoni akiwachapa wafuasi wake makofi.

 Katika video hiyo iliyosambazwa mitandaoni, pasta huyo anaonyeshwa akiwakung'uta waumini wake ambao waliokuwa wamepanga foleni. 

Mwanamke mmoja pia anaonekana akijaribu kumkimbia pasta huyo lakini alimufuata na kuendelea kumchapa huku akisema “enda chini…harakisha chini chini..lala chini..harakisha

Kulingana na video hiyo ambayo tarehe ya tukio hilo haikutambuliwa, haijabainika wazi chanzo cha hatua yake ama endapo ilikuwa njia ya kuwabariki waumini wake kwa kuwazaba makofi.

 Mnamo mwezi Agosti washiriki waumini kutoka kanisa hili walimshurutisha pasta huyo kuwaomba msamaha baada ya kuwatushia peupe kuwa atawanyofoa nyeti zao. 


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger