Thursday, 19 September 2019

Afikishwa Mahakamani kwa kumchoma mtoto mikono

...
Mkazi wa Makongo, Nicholaus Makali (32), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa kosa la kufanya ukatili dhidi ya mtoto (jina linahifadhiwa).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Ellen Masulali, alidai Agosti 25, mwaka huu eneo la Makongo DTV wilayani Ubungo, Dar es Salaam, Makali ambaye ni mlezi wa mtoto huyo wa miaka 10, alimchoma mikono yake na chuma na kumshambulia mara kadhaa kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Masulali alisema upelelezi haujakamilika, aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa tena kesi hiyo.

Hakimu Mwakalinga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, mmoja awe mfanyakazi katika taasisi inayotambulika kisheria, barua za utambulisho, nakala ya kitambulisho cha taifa na kusaini bondi ya Sh milioni tatu.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kwa kusikilizwa tena Oktoba Mosi.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger