Wednesday, 15 May 2019

Kisena Wa Udart Afutiwa Mashtaka

...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, leo Jumatano Mei 15, 2019 imewafutia mashtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar (UDA-RT), Robert Kisena na wenzake watatu.

Kisena na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji wa fedha na kuusababishia mradi wa UDART hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 2.41. 

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kulwa Kisena, Charles Newe na raia wa China, Cheni Shi.

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu91 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao hivyo hakimu Simba akaifuta.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger