Wednesday, 15 May 2019

GUMZO LA MFALME MSWATI WANAUME KUOA WAKE WAWILI LAIBUKIA KWENYE BUNGE LA AFRIKA…UKWELI HUU HAPA

...
Mbunge wa Bunge la Afrika kutoka Eswatini akizungumza katika Mkutano wa Bunge la Afrika unaoendelea Jijini Johannesburg,Afrika Kusini leo - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
 ****
Serikali ya nchi ya Eswatini imekanusha taarifa zinazoenea kwa kasi mtandaoni kuwa Mfalme Mswati III ametoa agizo la wanaume nchini humo kuanzia Mwezi Juni 2019 kuoa wanawake wawili au zaidi la sivyo unatupwa jela. 

Akizungumza leo asubuhi Jumatano Mei 15,2019 katika Bunge la Afrika linaloendelea jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini,Mbunge wa Eswatini, Mhe. Mike Temple amesema ni vyema taarifa hizo zikapuuzwa kwani zina lengo la kumchafua Mfalme Mswati III. 

“Mhe.Rais,kabla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Bunge la Afrika ya mwaka 2018 na bajeti iliyopendekezwa ya Bunge la Afrika kwa mwaka 2020,naomba kuweka sawa jambo moja ambalo linasambaa sana mtandaoni kuwa Mfalme wetu ametangaza kuwa wanaume waoe wanawake wawili au zaidi”,ameeleza Mhe. Temple. 

“Kwa niaba ya Mfalme wetu,naomba kuliambia bunge hili kuwa,Mfalme wetu siyo dikteta na haongozi kwa matamko,na hakuna sheria ya kumlazimisha mtu kuoa..hivyo hajasema na wala hategemei kusema hicho kinachoenezwa, huu ni uongo mtupu unaolenga kumchafua Mfalme wetu”,amesema Mhe. Temple. 

“Tuondoe huu upepo unaoenea na kuchafua nchi na Mfalme wetu,mimi mwenyewe hapa nina mke mmoja tu,na hakuna sheria inayomlazimu mtu kuoa, kuoa ni maamuzi ya mtu binafsi kuchagua kuoa au la”,ameongeza Mhe. Temple.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog 

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger