Na Mwandishi wetu Dodoma Wanawake wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020 wameanza kujengewa uwezo wa namna ya kushiriki na kushinda. Akizungumza katika mdahalo wa ushiriki wa wanawake kwenye uongozi ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), mkurugenzi wa mtandao huo, Lilian Liundi amesema ili kufikia usawa wa kijinsia kwenye uongozi, wanawake wenye nia ya kuingia madarakani lazima wajengewe uwezo. “Tumeshaanza mchakato wa kuwatambua wanawake wanaotia nia katika maeneo mbalibali Tanzania na program ya kuwajengea uwezo ipo tayari…
0 comments:
Post a Comment