Bodi ya filamu nchini imetangaza leo kumfungulia muigizaji Wema Sepetu baada ya kutumikia adhabu yake kwa muda wa miezi minne kutokana na kuvujisha video yake yenye maudhui ya ngono na kusambaa katika mitandao ya kijamii. Wema amesema amejifunza na hahitaji kurudi alikotoka ameshaumizwa sana na tabia zake ameahidi kubadilisha mwenendo wake. Hivyo Bodi ya Filamu imetoa uamuzi mbele ya vyombo vya habari kupitia kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce Fissoo, ambaye emesema imeamua kumfungulia Wema kwa sababu amefuata maelekezo aliyopewa na bodi hiyo kwa asilimia 75.…
0 comments:
Post a Comment