Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ambaye ni mwenyekiti wa kamati maalumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi, amewataka wakazi wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wenye migogoro ya ardhi na taasisi za jeshi na uwanja wa ndege kuwa watulivu, baada ya Rais John Magufuli kuagiza umalizwe. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Shibula wilayani humo, Lukuvi alisema Rais ameunda kamati hiyo kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa mitaa 11 na kupata ufumbuzi ambao utawezesha wananchi kulipwa fidia. “Hapa Mwanza mgogoro ni mkubwa sana baina…
0 comments:
Post a Comment