Wanafunzi wa chuo kikuu cha sua wakati wakiwa wanaelekea kumaliza muhula wao wa kwanza wa masomo tangu walipofungua mwezi wa kumi na moja mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana,kumetokea uhaba wa fedha baada ya kucheleweshewa pesa yao ya special faculty allowance ambayo inatakiwa alipwe mwanafunzi wakati tu akiwa amewasili chuoni.
tukizungumza moja kwa moja na mwanafunzi wa kozi ya aquaculture na toursim management (majina tumeyahifadhi) kwa wakati tofauti wamesema kwamba kiukweli hali ya kimaisha ni ngumu sana kwani hadi sasa hawajui watakula nini kwani wamekuwa wakishindia mkate na maji kwa ukosefu wa pesa.
Maswayetu blog team tulitinga ofisi za bodi ya mikopo ,kuulizia swala hilo na kuambiwa kwamba maelezo yote yapo chuoni kwani pesa zote zilishatolewa.
tutaendelea kufatilia swala hili na kukuletea majibu yaliyosahihi mara tutakapofika chuo husika na kupata maelezo kutoka kwa viongozi husika.
0 comments:
Post a Comment