MTOTO mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake.
Akipia stori na paparazi wetu juzi
jijini Dar, Jokate alisema anapenda mwanaume ambaye atajua kutafuta
fedha kwa nguvu zote, awe anajua kubembeleza na awe na nidhamu kwa
wazazi wake.
“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa
mtafutaji wa fedha, sipendi mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma
kwa kazi zake na kwa mpenzi au familia yake na pia ajue
kunibembeleza,’’ alisema Jokate.
0 comments:
Post a Comment