STAA wa
muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ambaye aliwahi kutangaza
kuacha fani ya maigizo na muziki amejikuta akiumbuka kwa mashabiki wake
kutokana na kuendelea kukomaa katika gemu kwa kuachia kazi mpya na
kuandaa matamasha mbali mbali.
Msanii huyo alitoa uamuzi huo kwa madai
kuwa alichoshwa na skendo za kila kukicha ambazo wakati mwingine
zimekuwa zikimshushia hadhi katika jamii, ikiwemo skendo ya kunaswa
kwenye mtego wa kujiuza ilioandliwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya
Global.
Akizungumza na paparazi wetu hivi
karibuni, Baby Madaha alisema hawezi kupinga kama alizungumza hayo
isipokuwa tangu atoe kauli hiyo amejikuta akizidi kupata mafanikio
makubwa katika muziki.
“Naweza kusema nimeumbuka kwa kile
nilichoongea, maana nimejikuta nashindwa kutekeleza nilichowaambia
mashabiki wangu sababu dili zinakuja, siwezi kuziacha,” alisema Baby.
0 comments:
Post a Comment