
Taarifa zilianza kusambaa kuwa mwanadada huyo kwa sasa ametumbukia katika tatizo la matumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada mkubwa.

Kupita ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.
Ray C ameandika kupitia Instagram >>> ‘Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasisi yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za dawa za kulevya nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine’

‘Moyoni nikawa nafikiria huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!!ikawa Kama bahati tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha dawa Mwananyamala! nilipomuona Doren kwa mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza tiba ya methadone, isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu nimechoka maisha ya utumwa nisaidie!!’

‘God We Trust!!!I love You my lil’ sister….. nawahamasisha wengine huko mliko mwenye ndugu, jamaa au rafiki njoo katika taasisi yetu uweze kusaidiwa! usikubali maisha ya utumwa wa dawa za kulevya, njoo tukusaidie… Ray C Foundation pamoja na kitengo cha Methadone We love you guys, We can help you….”
0 comments:
Post a Comment