Thursday 29 May 2014

NJAA NJAA NJAA"HAYA NI MANENO YA WANAFUNZI SUA-MARA TU NILIPOONANA NA MAPEMA LEO HII"

...
                                            


NJAA NJAA NJAA"HAYA NI MANENO YA WANAFUNZI SUA-MARA NILIPOONANA NAO" HUKU WENGINE WAKISEMA TUMECHOKA NA PASI NDEFU,WENGINE PIA WAKISEMA MAISHA MAGUMU.
HUKU WENGINE WAKISEMA "NITAWEZAJE KULA KWA FOLENI PECAM?",NA MWINGINE AKISEMA NITATUMIA MOZILA FIRE FOX HADI LINI???
                                               

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KILIMO SOKOINE KILICHOPO MJINI MOROGORO WANAISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KUTOKANA NA KUTOKUWA NA PESA YA CHAKULA.

WAKIZUNGUMZA KWA NYAKATI TOFAUTI BAADHI YA WANAFUNZI WA CAMPUS YA MAZIMBU NA MAIN WAMESEMA KUWA HADI SASA HAWAJUI HATIMA YAO NI NINI KUTOKANA NA KUTOKUWA NA HATA SENTI TANO YA KULA HUKU WAKIENDELEA KUMUOMBA MUNGU KILA SIKU WAAMKE VIZURI.


NILIBAHATIKA KUMHOJI MWANAFUNZI MMOJA WA KOZI YA INJINIA MWAKA WA NNE(jina tumehifadhi) AMBAE PIA ALISEMA KUWA NI CR WA DARASA HILO ALISEMA KUWA HADI SASA YEYE MWENYEWE AMEKUWA AKISHINDIA MKATE MAJI KWA SIKU NZIMA.

PIA MWANAFUNZI MWINGINE WA KOZI YA BVM MWAKA WA 3(jina tumehifadhi) ALISEMA KUWA YEYE BINAFSI HANA PESA ILA KUTOKANA NA KOZI YAO ILIVYO NGUMU HAWEZI KUGOMA KWANI KILA SIKU WALIMU WANAZIDI NKUINGIA DARASANI NA KUFUNDISHA HIVYO AKISEMA ASIINGIE DARASNI ANAWEZA KUFUKUZWA CHUO.

CHA KUSITISHA ZAIDI NI PALE NILIPOKUTANA NA BINTI KOZI YA HUMAN NUTRITION MWAKA WA TATU(tumehifadhi jina kwa usalama) AKISEMA KUWA KWA KUWA HANA PESA AMEKUWA AKIENDA KUTAFUTA WANAUME MAENEO YA SAMAKI SAMAKI NA KAHUMBA MJINI MOROGORO ILI  KUKIDHI MAHITAJI YAKE"
                                                          
BAAADA YA HAPO SIKUSITA KUONANA NA KIONGOZI WA MIKOPO NDUGU GETURDE AMBAE ALISEMA KUWA MAJIBU WALIYOPEWA KUTOKA UONGOZI WA CHUO UMESEMA KUWA HADI SASA HAKUNA PESA HIVYO WANAFUNZI WANATAKIWA WAWE WAVUMILIVU KUSUBIRIA PESA YAO YA CHAKULA.    

HATA HIVYO WANAFUNZI HAO WAMEKOPESHWA NA CHUO KWA KUKOPEWA CHAKULA CAFITERIA ILIYOPO CHUONI HAPO IITWAYO'pecam" AU FACEBOOK!

NILIMTAFUTA WAZIRI MWENYE DHAMANA NA ELIMU YA JUU KUZUNGUMZIA HILI AMBAE ALISEMA "TUNALITAMBUA HILI NA MDA SI MREFU VIJANA WATAPATA PESA YAO.

HADI TUNAKWENDA MITAMBONI HAKUNA SOLUTIONS MBADALA YA MATATIZO YA WANAFUNZI HAWA ILIYOKUWA IMEPATIKANA.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger