Friday 23 May 2014

BIBI ANASWA UWANJA WA NDEGE DAR AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA

...

Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei 15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa shaka na kumkamata.READ MORE>>>
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger