Friday 30 May 2014

WAPINZANI BUNGENI WAMKAANGA ZITTO

...


Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto Kabwe ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Hii ni mara ya kwanza kwa kambi ya upinzani kumhusiaha mbunge 'mwenzao' na tuhuma za ufisadi tofauti na kawaida yao ya 'kuwashughulikia' ubadhirifu katika Serikali.

Zitto, mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema na ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), anadaiwa kuchota fedha hizo kupitia kampuni ya Leka Dutigite ambayo ina hisa nyingi katika kampuni nyingine ya Gombe Advisors Limited ambayo Zitto ni mkurugenzi wake.
Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni jana kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mwaka 2014/15, waziri kivuli wa wizara hiyo, Joseph Mbilinyi alisema Zitto hakutakiwa kuchota fedha hizo kwa kuwa anabanwa na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Alisema Zitto, ambaye katika miezi ya karibuni aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa chama chake, ni mwenyekiti wa PAC, kamati ambayo jukumu lake ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika wizara na mashirika ya umma, yakiwamo Tanapa na NSSF, hivyo kulikuwa na mgongano wa kimasilahi katika suala hilo.
Tuhuma za Zitto
Katika hotuba yake, Mbilinyi alisema taarifa za kibenki ambazo kambi hiyo imezipata zinaonyesha kuwa Desemba 10, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha Sh12 milioni kwenda katika akaunti ya kampuni ya Leka Dutigite.
"Siku moja baadaye fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo. Januari 14 na Februari 7, 2013 akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh28.6 milioni," alisema Mbilinyi.
Sugu alisema fedha hizo ziliingizwa na mtu aitwaye Mchange na kwamba ilipofika Februari 7 zote zilikuwa zimetolewa.
Alisema Februari 28 mwaka jana, akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh32.3 milioni kutoka NSSF na kwamba siku hiyo hiyo fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadaye shirika hilo lilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite.
"Ziliingizwa Sh46.6 milioni ambazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Katika kipindi cha miezi mitatu, kati ya Desemba 10, 2012 na Machi 4, 2013 kampuni hiyo (ya Zitto) ililipwa Sh119.9 milioni kwa utaratibu huohuo wa ingiza-toa fasta," alisema Mbilinyi.
Alisema kati ya fedha hizo Sh12.2 milioni zililipwa na Tanapa na Sh79 milioni zililipwa na NSSF.
CHANZO:MWANANCHI
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger