Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Mwendesha Boda boda Idrisa Said Bayaga(32) wa Kituo cha waendesha pikipiki cha Nyerere Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya(mapenzi) tendo la ndoa(MAHARIMU)na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe mwenye umri wa (11).
Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu mfawidhi mwandamizi Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gosper Luoga.
Mwendesha mashtaka mwanasheria wa Serikali Gregoli Mhangwa ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe kwa nyakati tofauti kuanzia kipindi cha mwezi Aprili mwaka huu hadi mwezi Septemba .
Aidha kuwa kitendo hicho cha kufanya tendo la ndoa na mtoto wake mwenye umri mdogo wa miaka 11 ni kutenda kosa kinyume na kifungu cha sheria Namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019.
Mtuhumiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka hayo na mwanasheria wa Serikali alikana na mashtaka hayo ya kutenda kosa la kufanya tendo la ndoa kwa nyakati tofauti na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.
Baada ya mtuhumiwa kukana mashtaka hayo mwendesha mashtaka Gregoli Mhangwa aliiambia Mahakama kuwa upande wa mashtaka umeishakamilisha upelelezi wa kesi hiyo .
Hivyo aliiomba Mahakama iweze kuendelea na hatua zinazofuata za kimahakama kufuatia kukamilika kwa upelelezi uliofanywa na pande wa mashtaka .
Kufutia maombi hayo ya upende wa mashitaka Hakimu Luoga alikubaliana na hoja hiyo iliyotolewa mbele yake na upande wa mashitaka ambapo mtuhumiwa Idrisa Said Bayaga alisomewa hoja za awali za mashtaka .
Baada ya kutolewa mahakamani hapo hoja za awali kuwasilishwa Mahakani hapo Hakimu Mkazi mfawidhi Mwandamizi Gosper Luoga aliiambia mhakama kuwa mdhamana wa mshitakiwa upo wazi na anatakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyo hamishika na dhamana kuwa wazi Huku mtuhumiwa kushindwa kutimiza masharti hayo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo Desemba 5 itakapoanza kusikilizwa ambapo mtuhumiwa amekwenda rumande kwenye gereza la mahabusu la Mpanda Mjini.
Chanzo - Katavi Press club blog
0 comments:
Post a Comment