Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani pamoja na mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto wakiangalia Nguo zilizoshonwa na wahitimu wa fani ya Ushonaji.
Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog
CHUO cha Shinyanga Network Training Center (SHY NET) kilichopo katika Kata ya Lubaga Mkoani Shinyanga, kimefanya mahafali ya 1 chuoni hapo, kwa kuwaaga wahitimu wa mwaka wa pili kutoka fani mbalimbali.
Mahafali hayo yamefanyika chuoni hapo Novemba 17,2022, na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ,na Taasisi binafsi huku mgeni rasmi akiwa ni Diwani wakata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Reuben Dotto.
Akizungumza kwenye Mahafali hayo Mkuu wa chuo cha SHY NET Shinyanga Abubakar Rehani, amesema chuo hicho kilianzishwa mwezi January mwaka 2022,na kuanza kutoa fani 2 ambazo ni fani ya ufundi Umeme ,Ushonaji na ubunifu wa mavazi , lakini mpaka sasa chuo kinatoa kozi za muda mrefu pamoja na kozi zamuda mfupi.
Amesema chuo kilianza kikiwa na mwanafunzi mmoja lakini wamehitimu wanafunzi 12 wa kiume wakiwa 7 na wa kike 5, na kubainisha kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayopelekea wanachuo kushindwa kujisomea nyakati za usiku na barabara kushindwa kupitika kipindi cha mvua.
“Mgeni Rasmi chuo chetu kwa sasa tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme pamoja na ubovu wa miundo mbinu ya barabara ya kuja chuoni hivyo wanafunzi wengi kushindwa kujisomea nyakati za usiku na barabara kushindwa kupitika kipindi cha mvua”amesema Abubakari.
Pia, amesema changamoto nyingine ambayo inawakabili chuoni hapo, ni ukosefu wa huduma ya maji ambapo huingia gharama ya kuchimba visima na kutumia sora na jenereta wakati wa kusukuma maji.
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wazazi, kuwasaidia watoto wao ambao wanahitimu mafunzo mbalimbali ya ufundi chuoni hapo kwa kuwanunulia vifaa au kuwapatia fedha za mitaji ili wajiajiri wenyewe, kuliko kuwaacha wakilandalanda mitaani na kulalamika hakuna ajira na wakati wana ujuzi wa kutosha.
Aidha Mwanafunzi Catheline Leonard akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, amesema changamoto kubwa ambayo inawakabili wahitimu wa mafunzo ya ufundi ni ukosefu wa ajira na fedha za mitaji ili wapate kujiajiri wenyewe na ndiyo maana wengi wao huishia mitaani na kukaa bila kazi.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Reuben Dotto , amewatoa wasiwasi wahitimu wa SHY NET hasa wale ambao wanaishi Manispaa ya Shinyanga ,kuwa hakuna ugumu wowote wa kupata fursa zilizopo katika kata hiyo na Manispaa kwa ujumla kwa kuwa wana ujuzi unaweza kuwasaidia kujikwamua kimaisha.
Dotto ametoa ahadi pia kwa wahitimu wa fani ya umeme kuwa ataangalia namna ya kuwasaidia wale wanafunzi wa fani za umeme kwa kuwaombea kazi kwenye miradi mbalimbali ya manispaa hiyo ikiwamo ya ujenzi wa vituo vya afya, zahanati,Sekondari , huku akiwasihi wasione aibu kufungua ofisi yao na kujiajiri wenyewe hali itakayo wewezesha wahitimu kumudu soko la ushindani kwenye ajira, a
Akizungumzia suala la changamoto ya Umeme ,maji ,na barabara Dotto , amesema atafuatilia kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa kwa haraka ikiwemo kuhamasisha jamii kupeleka watoto wao wanao hitimu elimu ya kidato channe katika shule hiyo ili kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi katika kata hiyo na manispaa kwa ujumla.
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akitoa taarifa ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akitoa taarifa ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akimuongoza mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto na kumuonesha mazingira ya chuo.
Wahitimu mwaka wa Pili Chuo cha SHY NET wakimwelezea mgeni rasmi mbinu mpya ya kuunganisha umeme majumbani.
Mgeni rasmi Leuben Dotto pamoja na Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani wakisikiliza maelezo kutoka kwa wahitimu
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani pamoja na mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto wakiangalia Nguo zilizoshonwa na wahitimu wa fani ya Ushonaji .
Mgeni Rasmi Reuben Dotto akizungumza na wazazi na walezi pamoja na wahitimu kwenye mahafali ya Kwanza ya Chuo cha SHY NET.
Mhitimu Catheline Leonard akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wengine.
Wanachuo wa mwaka wa kwanza wakielezea ujuzi walio pata mpaka sasa katika fani ya umeme.
Wahitimu wa mahafali ya kwanza chuo cha SHY NET SHINYANGA wakiimba wimbo maalum
Wahitimu wakionesha mtindo wa mavazi.
Mhitimu akionesha mtindo wa mavazi.
Wahitimu wakionesha mtindo wa mavazi.
Miundo mbinu ya chuo
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akiwaonyesha mazingira ya chuo wageni waalikwa pamoja na wazazi .
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akiwaonesha mazingira ya chuo wageni waalikwa pamoja na wazazi .
0 comments:
Post a Comment