Benki ya CRDB baada ya kuhitimisha awamu ya kwanza ya kampeni yake ya “Tisha na TemboCard” na kuwakabidhi tiketi za kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia wateja wake watatu walioibuka washindi wa jumla wa kampeni hiyo hatimae yawapeleka Qatar.
Wateja hao waliondoka tarehe 25 kupitia uwanja wa Julius Nyerere International Airport na kusindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo.
Akizungumza kwaniamba ya washindi wenzake katika safari hiyo, Rajabu Dossa Mfinanga aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwapa kipaumbele wateja wake kwani wanajihisi ni sehemu ya familia ya Benki hiyo, pia alitoa rai kwa watanzania kujijengea utamaduni wa kutumia kadi zao za benki hiyo kwa kuafanya manunuzi na malipo mbalimbali kama bili, usafiri na kadhalika si kwasababu ya kushinda zawadi;
“Niwape wito wateja wenzangu wa Benki ya CRDB na watanzania kwa ujumla tujenge utamaduni wa kutumia kadi kupata huduma mbalimbali badala ya kutumia fedha taslimu. Matumizi ya kadi ni rahisi na inakupa kujiamini zaidi kuliko ukibeba fedha taslimu, unakosa kujiamini kila uendapo unakuwa na wasiwasi kwa kuhofia kuibiwa, lakini ukiwa na Tembocard yako mambo ni burdani”. Aliongeza Mfinanga.
Kwakufahamu namna ambavyo Watanzania wanapenda michezo na hasa msimu huu wa Kombe la Dunia imeona ni vyema ikawa sehemu ya kutimiza shauku ya wateja wao ya kushiriki katika mashindano hayo makubwa duniani.
Katika safari hiyo Benki ya CRDB imewagharamia tiketi za ndege kuelekea Doha Qatar, malazi, pamoja na fedha za matumizi wakiwa huko.
Washindi walioibuka kidedea kwenye safari hiyo ya kushuhudia kombe la dunia ni pamoja na; Haji Athumani Msangi, Erick Boniface Kashangaki, Kelvin Jackson Twissa, na Rajabu Dossa Mfinanga wote wakazi wa Dar es Salaam.
Benki ya CRDB inatarajia kuendesha awamu ya pili ya kampeni hii na kuahidi kuleta mambo mazuri zaidi, hivyo imetoa rai kwa wateja wake kuendelea kutumia kadi zao za TemboCard kulipia manunuzi ili kupata punguzo la bei (discount) au kurudishiwa sehemu ya kiasi walichotumia (cashback) katika maduka mbalimbali.
--
0 comments:
Post a Comment