Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limetoa mafunzo ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la polisi na askari polisi wa Dawati la Jinsia na Watoto ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Akifungua mafunzo kazini kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto leo Jumatatu Novemba 21,2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amewataka kuzingatia maadili ya kazi yao na kuchukua hatua za haraka wakati wakiwahudumia Waathirika/Madhura wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
“Ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ni lazima askari polisi wawe na maadili na kuepuka vitendo vya rushwa na kusuluhisha kesi za ukatili ili wale waliofanya makosa waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria”, amesema Kamanda Magomi.
“Askari polisi tunapopata kesi za ukatili wa kijinsia ni lazima tusimame katika haki, tutumie lugha nzuri kwa madhura wa ukatili wa kijinsia, tusiwe na mahusiano na wahalifu, tusisuluhishe kesi, tuzipokee, tuzipeleleze na kutenda haki. Wapelelezi fanyeni kazi kwa weledi. Wakuu wa vituo vya polisi msikae na kesi, msisuluhishe na zipelekeni hizo kesi za ukatili wa kijinsia kwenye dawati la jinsia na watoto”,amesema Kamanda Magomi.
Katika hatua nyingine Kamanda Magomi amesema watapita kwenye migodi ya madini ambako kuna taarifa za kuwepo matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo biashara ya ngono ambayo hadi watoto wanashiriki.
“Tumepata taarifa kuhusu kuwepo kwa matukio ya ukatili kwenye migodi midogo. Tukiwa tunaelekea kwenye Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huko migodini tutakwenda. Polisi tutafika kwa ajili ya kutoa elimu na kuwakamata wanaofanya ukatili wa kijinsia migodini”,amesema Kamanda Magomi.
Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo maafisa wa jeshi la polisi na Watendaji wa dawati la jinsia namna ya kushughulikia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto leo Jumatatu Novemba 21,2022 katika Bwalo la Polisi Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto.
Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere akizungumza kwenye mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto.
Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto wakiwa kwenye mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia.

0 comments:
Post a Comment