Tuesday 29 November 2022

WATOTO 521,025 KUPATIWA CHANJO YA POLIO SHINYANGA DESEMBA 1 - 4, 2022

...

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulutyu akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Novemba 29,2022. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wapatao 521,025 wanatarajia kupatiwa matone ya kuzuia ugonjwa wa Polio Mkoa wa Shinyanga kaya kwa kaya kuanzia Desemba 1 hadi 4,2022.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Novemba 29,2022 kuhusu maandalizi ya Kampeni ya utoaji wa matone ya chanjo ya Polio awamu ya nne, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulutyu amesema Mkoa wa Shinyanga umepokea jumla ya chanjo dozi 614,800 pamoja na vifaa vingine (marker pen, chaki, vipeperushhi, rejista) kwa ajili ya kufanikisha Kampeni hiyo.


"Mkoa wa Shinyanga ulitekeleza Kampeni ya Polio awamu ya tatu kwa mafanikio makubwa na kufikia kiwango cha utoaji kukiwa na ushiriki mkubwa wa wadau ambapo walengwa walikuwa 445,681 kuanzia Septemba 1 hadi 4,2022",amesema Mulyutu.


Mratibu wa Chanjo mkoani Shinyanga Timothy Sosoma, amesema Mkoa wa Shinyanga umeshapokea jumla ya dozi ya chanjo ya Polio 614,800 na walengwa wote watafikiwa na timu ya wataalam 1,021 lengo ni kufikia idadi ya watoto 521,025 ili kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulutyu akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Novemba 29,2022 kuhusu maandalizi ya Kampeni ya utoaji wa matone ya chanjo ya Polio awamu ya nne ikayofanyika kaya kwa kaya kuanzia Desemba 1 hadi 4,2022.
Mratibu wa Chanjo mkoani Shinyanga Timothy Sosoma akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio awamu ya Nne kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio kwa njia ya matone dhidi ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa juu ya kampeni ya utoaji Chanjo ya Polio kwa njia ya matone dhidi ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger