Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 kutoka Murang'a Kenya amezua gumzo mitandaoni baada ya kusimulia alivyoibiwa shilingi 700,000 na mpenzi wake.
Mwanamume huyo, Tom Waithaka Ikonya akisimulia kwa kilio na majuto alianzia kwa kusema kuwa angetaka masaibu yake kuwa funzo kwa vijana wadogo.
Ikonya mnamo Novemba 17 aliamua kwenda baa moja eneo la Maragua kaunti ya Murang’a kujiburudisha kwa siku mbili kisha kufika jijini kwa ajili ya kuanzisha biashara ya kuuza nyama.
Baada ya vileo kadhaa aliamua kutafuta chumba cha kukodi kulala bila mafanikio. Hapo alipatana na mwanadada mmoja aliyesema kuwa angempa pahali pa kulala.
Ikonya alizidi kusimulia na kusema alijaribu kuonywa na marafiki aliokuwa amewanunulia pombe ila baada ya kuwaza na kuwazua aliamua kwenda kulala kwa mwanadada huyo ambaye hakumjua.
Nyumbani kwa mpezi huyo alikula akaoga na akaamua kulala kama mfalme kwa siku 4.
Baada ya mazungumzo ya kujuana Ikoja alimwelezea nia yake ya biashara. Mwanadada huyo alimwahidi kwamba angempunguzia mzigo wa kutafuta pahali kuazisha biashara mradi tu amwamini.
Ikonja asijue hatari aliyokuwa amejiingiza, alimpa shilingi laki 7 za kusimamia bajeti ya biashara, mapato ya iwapo biashara ingeanza kwenda mrama na akamwongezea shilingi 50,000 kwa jambo mwanadada huyo alilolitaja la dharura.
Baada ya wiki moja baada ya kujuana "Nilimpa kadi ya ATM kutoa pesa hizo na kunirudishia, sikuhisi chochote kibaya kingetokea. Pia niligundua kuwa kuna kifurushi alichoacha na kilikuwa na nguo zangu. Sikufikiria sana. Niliendelea kuagiza pombe na kunywa," Ikonya alizidi kusimulia kwenye jarida hilo la Nation lililochapishwa mnamo Novemba 22.
"Nilipewa bili ya shilingi 3,100 kwenye hiyo baa na sikuwa na pesa ingine mfukoni mwangu. Pesa iliyobaki ilikuwa kwa mwanamke huyo," anasema.
Msichana huyo alikawia sana bila ya kurejea bila kujua likoenda. Ikonja aliamua kwenda kutoa pesa na kadi yake kwenye ATM.
"Kwenye ATM, alipatwa na mstuko alipoambiwa na mashine kwamba hana fedha za kutosha za kutoa shilingi 10,000 na baki yake ni shilingi 8 pekee," Mzee alisema.
0 comments:
Post a Comment